Pata taarifa kuu
EU-WAHAMIAJI-USALAMA

EU yapitisha mgawanyo wa wakimbizi 120,000, nchi nyingi za Mashariki bado zinasita

Nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimepitisha Jumanne wiki hii kwa "idadi kubwa" mgawanyo wa wakimbizi 120,000 barani Ulaya, na kupingwa na nchi nne za Mashariki kwa idadi iliyopendekezwa na Brussels.

Askari polisi wa Croatia mbele ya wahamiaji wanaosubiri kuingia katika kituo cha mapokezi cha muda cha Opatovac, Septemba 22, 2015.
Askari polisi wa Croatia mbele ya wahamiaji wanaosubiri kuingia katika kituo cha mapokezi cha muda cha Opatovac, Septemba 22, 2015. AFP | AFP
Matangazo ya kibiashara

" Uamuzi juu ya kuhamishwa kwa watu 120,000 umepitishwa na idadi kubwa ya nchi wanachama", imepongeza kwenye Twitter Ofisi ya Rais wa Luxemburg, ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya.

Tume ya Ulaya, kupitia pendekezo hilo, ambayo imezigawa nchi za Ulaya imepongeza "uamuzi huo muhimu. "

Uamuzi huo umechukuliwa na idadi kubwa ya nchi zilyoshiriki kikao hicho na kupingwa na Jamhuri ya Czech, Hungary, Romania na Slovakia ambazo zimepiga kura ya kupinga. Mjumbe wa Finland hakutoa msimamo wake. Poland, ambayo mpaka sasa ilikuwa moja ya nchi za kambi ya upinzani, imejiunga na kambi ya walio wengi.

" Hivi karibuni, tutagundua kwamba mfalme hana uamzi. Utaratibu mzuri umepotea leo", waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Czech, Milan Chovanec, amelaumu kwenye Twitter.

" Baadhi watasema kwamba Ulaya imegawanyika kwa sababu hatukufikia uamzi kwa makubaliano lakini tuko katika hali ya dharura ", amesema waziri wa Uhamiaji wa Luxemburg, Jean Asselborn, mkandarasi mkuu mazungumzo.

" Ilikuwa ni lazima leo kupitisha nakala hii ya kisheria, bila hivyo Ulaya ingegawanyika zaidi ", Jean Asselbom amebainisha.

" Ulaya imechukua majukumu yake kwa wakimbizi ", amesema Rais wa Ufaransa Francois Hollande, ambaye yuko ziarani mjini London, nchini Uingereza.

Hatua ya dharura iliyopendekezwa na Tume ya Ulaya inahusu wakimbizi 120,000 kutoka Syria, Iraq na Eritrea waliowasili tangu mwishoni mwa mwezi Agosti nchini Ugiriki na Italia, nchi ambazo ziko kwenye mstari wa mbele kwa kukabiliwa na mgogoro wa uhamiaji katika bara la kale tangu mwaka 1945.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.