Pata taarifa kuu
UJERUMANI-ULAYA-WAKIMBIZI-USALAMA

Wakimbizi: Ujerumani yafunga "kwa muda" mipaka yake na Austria

Ujerumani iliamua Jumapili Septemba 13 kufunga kwa muda mipaka yake siku moja kabla ya mkutano wa Jumatatu mjini Brussels ambao watashiriki mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya.

Baada ya kuuzidiwa na wimbi la wakimbizi, Ujerumani imetangaza kuwa inafungwa kwa muda mipaka yake na Austria, Septemba 13, 2015.
Baada ya kuuzidiwa na wimbi la wakimbizi, Ujerumani imetangaza kuwa inafungwa kwa muda mipaka yake na Austria, Septemba 13, 2015. REUTERS/Michaela Rehle
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unahusu jinsi ya kugawana idadi sawa ya wakimbizi. Mamia ya askario polisi wa Ujerumani wametumwa, hasa katika mji wa Bavaria, ili kudhibiti watu kutoka Austria.

Baada ya sera za kulegeza hatua kadhaa, taarifa hii kwa sasa inaashiria hatua kali za serikali dhidi ya wakimbizi. Katika mji wa Munich, ambapo wakimbizi 4500 waliwasili Jumapili hii.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Thomas de Maizière, ametangaza Jumapili hii kwamba nchi yake imeanzisha “ kwa muda ” utaratibu wa ukaguzi kwenye mipaka yake ili kudhibiti wimbi la wakimbizi wanaoingia Ujerumani.

“ Ujerumani imeanzisha kwa muda utaratibu wa ukaguzi kwenye mipaka yake, hasa kwa Austria “, ametangaza waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, wakati ambapo mji wa Munich, lango kuu la kuingila wakimbizi nchini Ujerumani, umeanza kuzidiwa na wingi wa wakimbizi, baada ya wakimbizi 63,000 kuwasili mjini humo kwa muda wa wiki mbili pekee.

Ujerumani haiko tayari tena kukubali kuwa wakimbizi wanaoingia kwa waingi barani Ulaya wanaweza "kuchagua" nchi itakayowapokea, pia ameonya Bw de Maizière.

“ Wakimbizi wanaomba hifadhi wanapaswa kufahamu kwamba hawatakiwi kuchagua nchi ambazo zitawapa hifadhi ”, waziri Maizière amewaambia waandishi wa habari, wakati ambapo nchi yake inasubiri kuwapa hifadhi wakimbizi 800,000 mwaka huu.

" Sheria za Ulaya, ambazo zinaamuru kuwa maombi ya ukimbizi yanatakiwa kuwasilishwa katika nchi ya kwanza ya Umoja wa Ulaya unapoingia barani Ulaya, zinapaswa kuendelea kufanya kazi ", ameongeza waziri Maizière.

Wakati hayo yakijiri hali hii ya wakimbizi wanaoelekea kwa wingi Ulaya inaendelea kusababisha vifo. Watu thelathini na nne, ikiwa ni pamoja na watoto wa changa wanne na watoto wenye umri wa miaka kumi na moja, wamekufa maji Jumapili hii baada ya boti waliokuwemo kuzama katika bahari ya Mediterranean katika mwambao wa kisiwa cha Farmakonis nchini Ugiriki, kilomita 15 kutoka pwani ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.