Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Uturuki: wanajeshi wengi wauawa katika shambulizi la waasi wa PKK

media Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, Julai 24, 2015 Ankara AFP/AFP/Archives

Askari wengi wa Uturuki wameuawa na wengine kujeruhiwa Jumapili mwishoni mwa wiki hii katika mashambulizi makubwa yaliyohusishwa waasi wa Kikurdi wa PKK, Kusini mashariki mwa Uturuki, vyombo vya habari nchini humo vimearifu.

Idadi ya askari ambao walipoteza maisha katika mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa Daglica haikutajwa lakini Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ameitisha kikao usalama cha dharura katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, mkutano ambao watashiriki viongozi wa kuu wa kiraia na kijeshi.

Bw. Davutoglu ameondoka haraka mji wa Konya, mji ulio katikati mwa Uturuki ambako alikua akihudhuria mechi ya soka kati ya Uturuki na Uholanzi, na kuelekea mji mkuu.

Katika mahojiano na truninga binafsi ya A Haber, Rais Recep Tayyip Erdogan amesema amepigwa na "mshangao" na shambulio hilo, bila hata hivyo kutoa idadi ya askari waliouawa au kujeruhiwa. rais Erdogan amebaini kwamba shambulizi hilo limetolkea wakati wa operesheni ya "kusafisha" iliyokua ikiendeshwa na vikosi vya jeshi dhidi ya ngome za waasi wa PKK.

" Hali ya hewa haikuwa nzuri katika eneo hilo. Tukio hilo lilitokea wakati wa kusafisha. Shambulizi la bomu la kutegwa ardhini lilitekelezwa ", mesema rais Erdogan, huku akiahidi kutoa jibu la haraka sana na lenye maamuzi.

" Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa majeshi ni ya kutusikitisha ", ameongeza Rais wa Uturuki.

Ndege za kivita za Uturuki zimeshambulia ngome kadhaa za waasi katika eneo hilo lilioko kwenye mpaka na Iraq, runinga ya NTV imearifu.

Ankara ilianzisha mwezi Julai operesheni kabambe " dhidi ya ugaidi" kwa waasi wa Kikurdi, na kusitisha makubaliano ya miaka miwili ya usitishwaji mapigano.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana