Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Maelfu ya wahamiaji waelekea Austria kwa mguu

media Maelfu ya wahamiaji waondoka kwa mguu kutoka kituo kikuu cha treni cha Budapest wakielekea kwenye mpaka wa Austria, Septemba 4, 2015. AFP/AFP

Maelfu ya wahamiaji wameondoka mapema leo Ijumaa alasiri kutoka kituo kikuu cha treni cha Budapest wakijaribu kutembea kwa mguu wakielekea "Austria", baada ya viongozi wa Hungary kuchukua uamzi Jumanne wiki hii wa kusimamisha usafiri wa kimataifa kwa kutumia reli, ameshuhudia mwandishi wa AFP.

Wahamiaji, ambao baadhi yao walikuwa wamekwama katika mji mkuu wa Hungary kwa siku kadhaa, wamesema wanataka kutembea kwa mguu hadi kwenye mpaka wa Austria, ulio kwenye umbali wa kilomita 175, wakati serikali ya Budapest imeongeza jitihada za kuwahamisha kinyume na matakwa yao katika makambi ya mapokezi ya kwanza.

Wahamiaji, ikiwa ni pamoja na watoto na watu wanaotumia viti vya magurudumu, wamevuka moja ya daraja kuu katika mji wa Danube bila hofu ya kukamatwa na vikosi vya usalama.

Hungary, moja ya nchi kuu wanakopitia wahamiaji kwa kwenda Ulaya ya Kati, kuulionekana wahamiaji wapya 3,300 wakiwasili kwa siku moja pekee ya Alhamisi, shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi limebaini leo Ijumaa.

Wakati huo huo Aylan, mtoto mdogo kutoka syria aliyefariki baada ya kuzama katika bahari wakati alipokua akijaribu kukimbia kufuatia mapigano nchini Syria, amezikwa le Ijumaa na familia yake, lakini tukio hilo la kusikitisha ambalo ni ishara kwa mgogoro wa wahamiaji limeendelea kuzua migawanyiko kati ya nchi za Ulaya.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana