Pata taarifa kuu
UYAYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Ulaya yashuhudia wimbi la wahamiaji haramu

Idara inayoshughulikia maswala ya mipaka barani Ulaya imetoa ripoti inayoeleza kuwa wahamiaji 107,500 waliingia barani Ulaya mwezi uliopita.

Makubaliano yanaeleza kipengele cha usalama wa eneo la Calais, ili kuzuia wahamiaji kuingia nchi Ufaransa kupitia njia za ardhini.
Makubaliano yanaeleza kipengele cha usalama wa eneo la Calais, ili kuzuia wahamiaji kuingia nchi Ufaransa kupitia njia za ardhini. REUTERS/Pascal Rossignol
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaonesha ongezeko la wahamiaji hao wanaoingia barani Ulaya wakitumia usafiri wa maji katika Bahari ya Mediterranean na idadi hiyo imeongezeka toka elfu 70 mwezi Juni.

Umoja wa Ulaya unasema kuwa hali hii ni hatari na ya dharura na mataifa yote ya Umoja huo yanastahili kunesha uungwaji mkono kwa mataifa yanayochukua jukumu la kuwakaribisha wahamiaji hao katika nchi zao.

Wakati ripoti hii ikitolewa, Italia ambayo hupokea wakimbizi wengi imesema imewakamata watu 8 ambao wanashukiwa kuwa katika mstari wa mbele kuwasafisha wahamiaji hao.

Katika hatua nyingine, raia sita wa Syria akiwemo mtoto wameripotiwa kuzama maji katika pwani ya nchi ya Uturuki walipokuwa wakijaribu kuingia nchini Ugiriki.

Umoja wa Ulaya utatumia Euro Bilion 2 nukta 4 kuziunga mkono nchini zinazowapokea wakimbizi hao wengi kutoka barani Asia na Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.