Pata taarifa kuu
UGIRIKI-WAHAMIAJI-UCHUMI

Zoezi la mapokezi laboreshwa Kos, lakini hali bado ni tete

Hali katika kisiwa cha Kos nchini Ugiriki bado ni tete: leo Ijumaa asubuhi, mamia ya wakimbizi, wengi wao kutoka Syria, wamewasili tena kwenye fukwe ya kisiwa cha Kos, wakitokea Uturuki.

Wakimbizi, wengi wao kutoka Syria, mbele ya uwanja wa taifa mpira wa Kos, wakisubiri utaratibu wa kujiandikisha.
Wakimbizi, wengi wao kutoka Syria, mbele ya uwanja wa taifa mpira wa Kos, wakisubiri utaratibu wa kujiandikisha. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao wanatazamiwa kujiandikisha mbele ya viongozi wa kisiwa hicho. Baada ya ghasia ziliozuka siku za hivi karibuni, hali ya utulivu imeanza kurejea, baada ya idadi ya askari polisi kuongezwa ili kukabiliana na wingi wa wakimbizi. Na Alhamisi, Agosti 13, kwa mara ya kwanza tangu mwanzo mwa wiki hii, zoezi la mapokezi limekua likifanyika katika mazingira ya kutatanisha.

Mbele ya milango ya uwanja mdogo wa mpira, kulikua na foleni mbili za watu, moja kwa wanawake na watoto, na nyingine kwa wanaume. Pembezoni, wahamiaji wao wenyewe ndio wamekua wakihusika na kutoa ulinzi, ili kuepuka, kama walivyosema, wingi wa watu na makabiliano kati ya wakimbizi na polisi ya Ugiriki.

" Najaribu kuandaa watu, kuwaweka sawa. Tumekua tukiwapanga watu kwa makundi, kama tulivyoombwa na polisi. Tunataka zoezi hili lifanyike kwa haraka, ili tuweze kuondoka hapa. Kwa upande wangu ni vizuri, kwa sababu hapa ninapoteza pesa nyingi, nguvu zangu, bila matokeo yoyote ", amesema mmoja wa wakimbizi hao.

Wahamiaji hao ni kutoka nchi nyingi, wengi wao ni kutoka Syria. Wote wamekua wakijaribu kuingia uwanjani, huku wakizuiliwa na polisi wa kutuliza ghasia, amearifu mwandishi wetu katika kisiwa cha Kos, Daniel Vallot. Matumaini yao: kupata ruhusa ya kuondoka Kos, ili waweze kujielekeza Athens.

Maelfu ya wahamiaji wamewasili miezi ya hivi karibuni katika bahari Aegean. Kutokana na ongezeko hilo la wahamiaji haramu, viongozi wa Ugiriki wamesema kuwa wamezidiwa na hali hiyo.

Uthibitisho kwamba hali hiyo imekua mbaya zaidi, Jumanne wiki hii, ghasia zilizuka kati ya wahamiaji katika kisiwa cha Kos. Wakiwatawanya kwa kurushiwa gesi pamoja na kupigwa fimbo, vikosi vya usalama vilijaribu kurejesha udhibiti wa hali hiyo.

Wahamiaji na wakimbizi 1,500 walikusanyika Jumanne wiki hii katika uwanja mdogo wa mpira katika kisiwa cha Kos nchini Ugiriki. Watu hao ikiwa ni pamoja na wanaume, wanawake na watoto wenye asili ya Syria wangelipaswa kujiorodhesha kwa viongozi wa kisiwa hicho wakati, kwa sababu ambazo bado hazijawekwa wazi, hali ilikua tata kwa vurugu kati ya wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.