Pata taarifa kuu
UGIRIKI-WAHAMIAJI-UCHUMI

Wahamiaji: hali ni tata katika kisiwa cha Kos, Ugiriki

Maelfu ya wahamiaji wamewasili miezi ya hivi karibuni katika bahari Aegean. Kutokana na ongezeko hilo la wahamiaji haramu, viongozi wa Ugiriki wamesema kuwa wamezidiwa na hali hiyo.

Polisi wa Ugiriki wa kuzima ghasia wakikabiliana na maelfu ya wahamiaji katika uwanja mdogo wa mpira katika kisiwa cha Kos, Agosti 11 mwaka 2015.
Polisi wa Ugiriki wa kuzima ghasia wakikabiliana na maelfu ya wahamiaji katika uwanja mdogo wa mpira katika kisiwa cha Kos, Agosti 11 mwaka 2015. REUTERS/ Yannis Behrakis
Matangazo ya kibiashara

Uthibitisho kwamba hali hiyo imekua mbaya zaidi, Jumanne wiki hii, ghasia zilizuka kati ya wahamiaji katika kisiwa cha Kos. Wakiwatawanya kwa kurushiwa gesi pamoja na kupigwa fimbo, vikosi vya usalama vilijaribu kurejesha udhibiti wa hali hiyo.

Wahamiaji na wakimbizi 1,500 walikusanyika Jumanne wiki hii katika uwanja mdogo wa mpira katikaa kisiwa cha Kos nchini Ugiriki. Watu hao ikiwa ni pamoja na wanaume, wanawake na watoto wenye asili ya Syria wangelipaswa kujiorodhesha kwa viongozi wa kisiwa hicho wakati, kwa sababu ambazo bado hazijawekwa wazi, hali ilikua tata kwa vurugu kati ya wahamiaji.

Polisi iliingilia kati kwa kuwapiga fimbo wahamiaji ho kabla ya hali kurejea kuwa shwari. Askari polisi wengine walipiga mabomu ya kutoa machozi karibu na eneo kulikokua kukishuhudiwa vurugu hizo. Picha, zilizopigwa zinaonesha wazi jinzi gani hali ilivyokua katika kisiwa hicho cha Kos.

Karibu wahamiaji 7,000 na wakaazi 30 000

Kufuatia tukio hilo, Meya wa Kos, Giorgos Kiritsis, ametoa wito, huku akivitaka vikosi vya usalama kukomesha vurugu hizo, zisitokei tena. " Damu zinaweza kumwagika ", Giorgos Kiritsis ameandika katika barua aliotuma kwa serikali mjini Athens akiomba msaada kufuatia hali hiyo.

Wahamiaji 7,000 kwa sasa wamepiga kambi katika kisiwa cha Kos, chenye wakaazi 30,000. Tume ya Ulaya imetangaza kutoa kiasi cha Euro milioni 500 kwa kipindi cha miaka sita ili kusaidia Ugiriki kusimamia mgogoro wa uhamiaji. Tangu mwanzoni mwa mwaka, wahamiaji 124,000 waliingia nchini Ugiriki na kupelekea ongezeko la 750% ikilinganishwa na mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.