Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Ulaya

Hali ya taharuki yatanda Uturuki, baada ya mashambulizi mengi

media Vikosi maalum vya Uturuki vikiiingilia kati wilayani Sultanbeyli mjini Istanbul, Agosti 10 asubuhi mwaka 2015, baada ya mashambulizi mawili kwenye ubalozi mdogo wa Marekani na kwenye kituo cha polisi. AFP PHOTO / OZAN KOSE

Mashambulizi mengi yametokea Jumatatu asubuhi wiki hii nchini Uturuki. Watu wasiojulikana waliufyatulua risasi ubalozi mdogo wa Marekani, mjini Istanbul, bila hata hivyo kusababisha majeruhi.

Hata hivyo shambulio la gari iliotegwa bomu limelenga kituo cha polisi upande wa Asia mjini. Askari polisi amefariki papo hapo. Wakati huo huo askari polisi wanne wa Uturuki wameuawa na vilipuzi viliowekwa kando ya barabara ya Kusini Mashariki mwa Uturuki, vyombo vya habari vya uturuki vimetangaza.

Shambulio baya lililosababisha vifo vingi limetokea katika wilaya ya Silopi, katika jimbo la Sirnak, kwenye mpaka na Iraq na Syria, limetangaza shirika la habari la kibinafsiDogan likinukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP. Vilipuzi viliowekwa barabarani vimewaua askari polisi wanne. Shambulio hilo limedaiwa kutekelezwa na waasi wa Kikurdi wa PKK.

Wakati huo huo mwanajeshi wa Uturuki ameuawa wakati waasi wa Kikurdi walishambulia kwa roketi helikopta ya jeshi iliokua ikibeba wafanyakazi katika sekta ya Beytussebap katika jimbo la Sirnak, kwa mujibu wa vyanzo hivyo. Jeshi la Uturuki limejibu mashambulizi hayo kwa kudondosha mabomu kwenye ngome za waasi wa Kikurdi wa PKK katika Ukanda huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana