Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-PKK-NATO-USALAMA

Ankara yaendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa PKK

Awali ilifahamika kuwa Uturuki imekua ikiendesha mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za kundi la Islamic State nchini Syria na wapiganaji wa Kikurdi (PKK) nchini Iraq.

Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015.
Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Lakini jeshi la Uturuki limeanza pia mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za wapiganaji wa Kikurdi katika aridhi yake. Mashambulizi mapya yametishiwa kuendesha Jumanne wiki hii.

Ingawa hii si mara ya kwanza ya aina yake tangu mwanzo wa kampeni hii ya mashambulizi ya angani, yanayolenga kwa wakati mmoja kundi la Islamic State na ngome za wapiganaji wa Kikurdi (PKK), Waziri mkuu aliwahi kutaja mashambulizi hayo " nchini Uturuki na nje ya Uturuki " bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Jambo jipya sasa ni kwamba uongozi ewa kijeshi nchini Uturuki unawasiliana katika shughuli hizi. Historia pengine ya kuonyesha dhamira ya vikosi vya majeshi ya ya Uturuki katika vita dhidi ya waasi.

Kama ni rahisi kupata taarifa juu ya hasara inayotokana na mashambulizi haya wakati yanapoendeshwa nchini Iraq, hata hivyo, upande wa Uturuki, ambapo hakuna uhakiki huru unaowezekana, ni vigumu kujua hasara inayotokana na mashambulizi hayo.

Lakini jeshi la Uturuki limesema kuwa limefikia malengo yake kwa asilimia 100. Maeneo yaliolengwa, kama siku ziliopita, ni katika milima ya juu ya mikoa ya Sirnak na Hakkari.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Istanbul, Jérôme Bastion, NATO inataka Ankara kulinda mchakato wa amani ilioafikiana na Wakurdi mwaka 2012. Lakini tangu Jumanne na kauli za rais wa Uturuki ambaye anaona kuwa "haiwezekani" kuendelea na mazungumzo, matarajio ya kupatikana kwa amani yameanza kupungua kwa kasi. Kauli za Erdogan zifanana na tangazo la kuvunjika kwa mchakato na PKK.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.