Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-PKK-NATO-USALAMA

Uturuki yaitolea wito Nato kuzungumzia suala la IS na PKK

Uturuki imeitisha mkutano wa dharura na wanajeshi wa kujihami kutoka nchi za Magharibi NATO, baada ya kuanza mashambulizi dhidi ya Islamic State.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisema hatokubaliana na mashambulizi ya kundli la Wakurdi la PKK na IS kufanya mashambulizi nchini mwake.
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisema hatokubaliana na mashambulizi ya kundli la Wakurdi la PKK na IS kufanya mashambulizi nchini mwake. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma lililopita, Uturuki ilianza kutekeleza mashambulizi ya angaa dhidi ya Islamic State nchini Syria na katika kambi za kundi la wapiganaji wa Kikurdi PKK Kaskazini mwa Iraq.

Mashambulizi haya yanakuja baada ya kundi la Islamic State kutekeleza shambulizi la kujitoa mhanga katika mpaka wa nchi yake na Syria juma lililopita na kusababisha vifo vya watu 32.

Msemaji wa kundi la Kikurdi Kaskazini mwa Iraq amethibitisha kutokea kwa mashambulizi hayo ya kijeshi katika kambi zao mbili katika eneo la Dohuk.

NATO imesema, Uturiki kama nchi inayotoa majeshi yake katika muungano huo ina haki ya kuitisha kikao hicho ikiwa inahisi kuwa imevamiwa katika mipaka yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.