Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-MASHAMBULIZI-USALAMA

Uturuki: mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa PKK Iraq

Ndege za jeshi la anga la Uturuki zimeruka Jumapili usiku mwishoni mwa juma hili kwa wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya ngome kuu za waasi wa Kurdistan (PKK) kaskazini mwa Iraq, vimearifu vyombo vya habari vya Uturuki.

Wilaya Gazi, mjini Istanbul, imekumbwa na maandamano ya vurugu yaliosababisha kifo cha askari polisi mmoja Jumapili Julai 26 wakati ambapo Ankara ilishambulia kwa mara nyingine tena ngome za PKK.
Wilaya Gazi, mjini Istanbul, imekumbwa na maandamano ya vurugu yaliosababisha kifo cha askari polisi mmoja Jumapili Julai 26 wakati ambapo Ankara ilishambulia kwa mara nyingine tena ngome za PKK. AFP PHOTO / OZAN KOSE
Matangazo ya kibiashara

Wimbi la kwanza la mashambulizi, lililoendeshwa usiku wa siku ya Ijumaa Julai 24 hadi Jumamosi Julaia 25, lilipelekea kusitishwa kwa mapigano kati ya Ankara na kundi la waasi, ambalo lilidai kutekeleza shambulio la kujitoa mhanga lililowaua wanajeshi wawili Jumamosi usiku, kusini-mashariki mwa Uturuki.

Jumamosi Julai 25 ndege za Uturuki ziliendesha mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria na dhidi ya kundi la waasi wa Kikurdi (PKK). Hali hii imewaghadhabisha viongozi wa Kikurdi nchini Iraq na wamefungua njia ya uwezekano wa mashambulizi ya ya kulipiza kisase.

Hali ni tata kwenye ardhi ya Uturuki. Wanajeshi wawili waliuawa na wengine wanne walijeruhiwa Jumamosi usiku kufuatia mlipuko wa bomu lililokua limetekwa katika gari. Shambulio hilo lililenga msafara wa kijeshi katika jimbo la Diyarbakir, linalokaliwa na Wakurdi wengi.

Masaa kadhaa kabla ya shambulio hilo katika jimbo la Diyarbakir, kundi la waasi la PKK lilitishia kuvunja uamzi wa kusitisha mapigano uliotangazwa na waasi hao peke yao mwaka 2013. Jumatano Julai 22 kundi la waasi wa Kikurdi (PKK), lililowekwa katika kkwenye orodha ya makundi ya kigaidi na serkali ya Uturuki, lilikiri kuhusika na mauaji ya askari polisi wawili katika mji ulioko karibu na mpaka wa Syria, katika kulipiza kisasi kwa shambulio la kujitoa muhanga la Suruç, lililotokea Julai 20 na badala yake kuhusishwa kundi la kijihadi la Islamic State (IS)jihadi Islamic State Group (EI). Shambulio lililogharimu maisha ya watu 32, wengi wao wakiwa wapiganaji wa Kikurdi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.