Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Bunge la Ugiriki lapitisha mageuzi yaliyopendekezwa na wakopeshaji

Bunge la Ugiriki limepitisha mapema leo Alhamisi asubuhi mfululizo wa mageuzi yaliyoombwa na wakopeshaji wa Ugiriki katika utangulizi wa mpango mpya wa msaada, licha ya migawanyiko kadhaa katika kambi ya Waziri mkuu Alexis Tsipras.

Mbele ya Bunge, Waziri mkuu wa Ugiriki uamehakikisha kwamba makubaliano yaliyofikiwa na wakopeshaji yalilikuwa njia mbadala pekee ya kuondokana na inayoikabili Ugiriki au kuondoka katika nchi zinaotumia sarafu ya Euro.
Mbele ya Bunge, Waziri mkuu wa Ugiriki uamehakikisha kwamba makubaliano yaliyofikiwa na wakopeshaji yalilikuwa njia mbadala pekee ya kuondokana na inayoikabili Ugiriki au kuondoka katika nchi zinaotumia sarafu ya Euro. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Hakuna mtu aliyetarajia kwa matokeo kama hayo. Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, Bunge Kigiriki (Vouli), limepitisha kwa asilimia kubwa muswada wa sheria uliyodaiwa inadaiwa na wakopeshaji, ameshuhudia mwandishi wa RFI katika mji wa Athens, Romain Lemaresquier. Wabunge 229 wamepitisha nakala hiyo, sita hawakutoa msimamo wao na 64, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa waziri wa fedha Yanis Varoufakis na Spika wa bunge Zoe Konstantopoulou, wamepiga kura dhidi ya hatua hizo, ikiwa ni pamoja na ongezeko la VAT na mageuzi ya pensheni.

Jumla ya wabunge 32 wa Syriza, chama cha mrengo wa kushoto chenye msimamo cha Waziri mkuu, wamepiga kura dhidi ya kupinga, wakati 6 hawakutoa msimamo wao katika upigaji kura huu ulioendeshwa chini ya mvutano mkali, ambao ulitanguliwa na maandamano ya kupinga hatua za wakopeshaji, maandamano ambayo yamesababisha matukio kadhaa katikati ya mji wa Athens. Waziri mkuu, hata hivyo, ameweza kutegemea sauti ya mshirika wake wa muungano , chama cha mrengo wa kulia cha ANEL, na zile za vyama vya upinzani.

Kura zisiokuwa na ulazima, kwa mujibu wa Theodoros Fortsakis, wa chama cha New Democrasy. " Sheria imepitishwa kwa asilimia kubwa, ambayo imewajumuisha wabunge kutoka vyama viwili vinavyotawala na vyama vitatu vya upinzani. Na laajabu ni kwamba kulikuwa na kura 38 za wabunge kutoka vyama vinavyounga mkono serikali ambazo zimekuwa hasi au zimetupwa kapuni ", amesema Theodoros Fortsakis.

Sasa Alexis Tsipras atajadili na washirika wa Ugiriki wa Ulaya mpango wa tatu wa msaada kwa nchi yake na kutpewa Euro zaidi ya bilioni 80 kwa kukuza uchumi, urekebishaji na kulipa madeni wakopeshaji wake ECB na IMF.

Nakala hii ambayo tayari imepitishwa na Bunge la Ufaransa itaidhinishwa nchini Finland na Ujerumani hasa, nchi mbili zinazowakilisha mstari mgumu dhidi ya Athens. Ugiriki pia inasubiri kuwekwa kwenye msaada wa dharura wa nchi za Ulaya Alhamisi wiki hii ili kukidhi mahitaji yake mara moja, na kwenye msaada ambao benki zake zitakua na matumaini kutoka Benki kuu ya Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.