Pata taarifa kuu
CUBA-UFARANSA-DIPLOMASIA

François Hollande ziarani Cuba

Rais wa Ufaransa François Hollande ameifanya ziara ya kikazi nchini Cuba, ikiwa ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa tangu nchi ya Cuba kupata uhuru wake mwaka 1898.

Rais wa Ufaransa François Hollande akifanya ziara ya kikazi nchini Cuba, Jumatatu Mei 11. Ziara hii ni ya kihistoria.
Rais wa Ufaransa François Hollande akifanya ziara ya kikazi nchini Cuba, Jumatatu Mei 11. Ziara hii ni ya kihistoria. REUTERS/Alain Jocard/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo ya François Hollande inakuja wakati vikwazo viliyochukuliwa nchi ya Cuba vikianza kuondolewa.

Ufaransa inatafuta kujiweka sawa katika masuala ya uchumi na kisiwa hicho cha Amerika ya Kusini.

Rais wa Ufaransa ameeleza kuwa ziara hiyo ni ya kihistoria. François Hollande ni rais wa kwanza kutoka nchi za Magharibi kuwasili nchini Cuba tangu kudorora kwa mahusiano kati ya Marekani na Cuba.

Itafahamika kwamba hivi karibuni Marekani na Cuba vilifufua uhusiano wa kidiplomasia, baada ya kudororo kwa kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyiopita. Ufaransa ilipiga kura mara kadhaa kwa kuunga mkono Umoja wa Mataifa, ili Marekani iondoleye vikwazo Cuba. “ Tunapaswa kutumia fursa ya yale yaliyopita kwa kuwa wa kwanza kuanzisha mahusiano katika masuala ya uchumi na Cuba ”, François Hollande amelielezea jarida la Jumapili ( Journal du dimanche).

Mbali na mahusiano ya kidiplomasia na nia ya kudumisha uhusiano kati ya Ufaransa na Cuba, rais wa Ufaransa anapania kuanzisha uhusiano na Cuba katika masuala ya biashara. Makampuni ya Ufaransa huenda yakafanikiwa katika mahusiano hayo kati ya nchi hizi mbili. Hata hivyo Ufaransa inatazamia pia katika hatua ya pili, kujadiliana na Cuba kuhusu masuala ya haki za binadamu. Cuba imekua ikilaumiwa kuvunja haki za binadamu, na kujihusisha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya binadamu.

Baadhi ya viongozi na wamiliki wa makampuni ya Ufaransa wameandamana na Rais Hollande katika ziara hiyo nchini Cuba

Ufaransa inaiuzia Cuba nafaka, mbolea ya kilimo na vifaa vya usafiri. Makampuni sitini tayari sasa yanaendesha shughuli mbalimbali katika kisiwa hicho, ikiwa ni pamoja na Bouygues, Air France, Total na Pernod-Ricard. Pernod-Ricard ni mwekezaji wa kwanza katika Cuba chini ya kampuni ya Havana Club.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.