Pata taarifa kuu
UFARANSA-UFILIPINO-HALI YA HEWA-DIPLOMASIA

Rais wa Ufaransa ziarani Ufilipino

Rais wa Ufaransa, François Hollande, anatazamiwa kufanya ziara kikazi ya siku mbili nchini Ufilipino kwa kukabiliana dhidi ya ongezeko la joto.

François Hollande afanya ziara ya siku mbili Ufilipino.
François Hollande afanya ziara ya siku mbili Ufilipino. AFP PHOTO / NOEL CELIS
Matangazo ya kibiashara

Hii ni kwa mara ya kwanza rais wa Ufaransa akifanya ziara rasmi katika nchi yenye visiwa 7,100.

François Hollande ameichagua nchi hii kama hatua ya mwanzo ya mwaka wake wa uhamasishaji juu ya suala la hali ya hewa, mwaka ambao utakamilika kwa mkutano wa kilele kuhusu hali ya hewa duniani ambao utafanyika mwezi Desemba mwaka 2015 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Ufilipino ni mshirika wa karibu iliochaguliwa na Ikulu ya rais wa Ufaransa katika mtazamo wa mkutano wa kilele utakaofanyika Paris.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI, katika mji wa Manila, Anissa el Jabri, kimbunga Haiyan kinachokwenda kwa kasi ya zaidi ya kilomita 300 kwa saa, kilipiga Ufilipino mwishoni mwa mwaka 2013.

Zaidi ya watu 7,000 walifariki kutokana na kimbunga hiki, huku mamia ya maelfu wakijeruhiwa, na uharibifu mkubwa ukishuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hii. François Hollande amepanga kujielekeza nchini Ufilipino Alhamisi Februari 26, hasa katika mji wa Guiuan, mji wa kwanza uliyoathirika na kimbunga Haiyan ili kujionea mwenyewe hali ilivyo katika mji huo.

Ufilipino ni nchi ilioathirika lakini pia mtunzi wa mabadiliko ya tabianchi. Katika miaka ya hivi karibuni, Manila imewekeza katika kuzuia maafa, elimu na kilimo. Ni kwa mantiki hio, Ufilipino imechaguliwa kuwa " mshirika wa karibu wa Ufaransa".

" Ufilipino ni sauti ya maendeleo miongoni mwa nchi zinazoendelea", Ikulu ya Elyssé imebaini. Na sauti kama hizi, ndizo Paris inahitaji kwa ajili ya mafanikio ya mkutano kuhusu hali ya hewa utakaofanyika mwezi Desemba ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.