Pata taarifa kuu
UN-IS-MATEKA-USALMA-HAKI ZA BINADAMU

UN yaitaka IS kuwaachia huru mateka

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelitaka kundi la Islamic State kuwaachilia huru bila masharti mateka wote linalowashikilia.

Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, aprili 21 mwaka 2012.
Kikao cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, aprili 21 mwaka 2012. Reuters/Allison Joyce
Matangazo ya kibiashara

Wanachama hao 15 wa baraza hilo wamelaani mauaji ya mwandishi wa habari mmoja raia wa Japan baada ya kundi hilo kutoa mkanda wa video ulioneha wakimuua kwa kumkata kichwa raia huyo wa Japan.

Baraza hilo limesisitiza kuwa wote waliohusika katika mauaji ya Kenji Goto watawajibishwa, na kushinikiza kuachiliwa huru kwa mateka wengine wanaoshikiliwa na kundi hilo linalopigana nchini Iraq na Syria.

Wakati huo huo, Serikali ya Jordan, imeapa kufanya kila lilo ndani ya uwezo wake kuokoa maisha ya rubani Maaz al-Kassasbeh, ambaye ametekwa na wanamgambo wa IS baada ya ndege aliyokuwa anaendesha kuanguka mwishoni mwa mwaka jana nchini Syria.

Serikali ya Jordan na Japan zinasema hazitishwi na vitisho vya kundi hilo, wakati huu Islamic State ikitaka Jordan kumwachilia huru mwanachama wake la sivyo wataamua rubani wanayemshikilia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.