Pata taarifa kuu
VATICAN-PAPA-JAMII

Papa Francis awateua Makadinali wapya

Kiongozi wa Kanisa duniani Papa Francis amewateua Makadinali 20 wapya wengi wao kutoka bara la Afrika, Asia na Latin America.

Papa Francis awateua Makadinali wapya
Papa Francis awateua Makadinali wapya REUTERS/Alessandro Bianchi
Matangazo ya kibiashara

Makadinali 15 kati ya ishirini walioteuliwa wana umri wa chini ya miaka themanini na hivyo wanaingia katika kundi la Makadinali walio na jukumu la kumchagua kiongozi mpya wa kanisa hilo.

Askofu Soane Patita Paini Mafi kutoka Tonga mwenye umri wa miaka 53 anakuwa Kadinali mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa katika wadhifa huo.

Msemaji wa Vatican Father Federico Lombardi amesema hakuna Makadinali walioteuliwa kutoka Marekani na Canada kwa sababu nchi hizo zina Makadinali wa kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.