Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-Mapigano-Usalama-Sheria

Uturuki iko mbioni kuipa polisi uwezo wa kutosha

Serikali ya Uturki imewasilisha Jumatano wiki hii mswada wa sheria unaoipa polisi ya nchi hiyo uwezo wa kutosha baada ya maandamano ya wiki iliyopita ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini.

Polisi ya Uturuki ikipiga mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji wa Kikurdi, Septemba 29 mwaka 2014.
Polisi ya Uturuki ikipiga mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji wa Kikurdi, Septemba 29 mwaka 2014. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Mswada huu wa sheria unaeleza” mageuzi katika sekta ya usalama wa nchi”, ambao utajadiliwa wiki ijayo, utaipa polisi uwezo wa kutosha katika majukumu yake, hususan kuendesha msako, kusikiliza, kukamata na kuhoji watuhumiwa pasina ushahidi wowote kwa msingi tu kuwashuku.

“ Nakala hii inalenga kuipa uwezo polisi wakati kunajitokeza machafuko”, viongozi wamebaini. Lakini nakala hii inaonekana kama ni njia moja wapo ya kuwanyamazisha wpinzani wa Kikurdi.

Ibara zote za na kala hii, ambayo itajadiliwa katika kamati na kujadiliwa pia katika Bunge kabla ya kupitishwa, ni wazi kwamba zimeandaliwa dhidi ya wanaotuhumiwa kushirikiana na waasi wa Kikurdi.

Serikali inataka kuimarisha zaidi vyombo vya usalama, huku ikiendelea kunyooshewa kidole kwamba imekua ikitaka kuingiza Uturuki katika tawala za kiimla za miaka 1990.

Mswada huo wa sheria unalenga kuwakandamiza Wakurdi waliokasirishwa na vikwazo vya Kobane na ambao wakiwa tayari kukemea vikali mbinu za serikali ya Ankara za kutaka kuvunja mchakato wa amani. Hali hiyo imezua mfarakano nchini Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.