Pata taarifa kuu
UFARANSA-Siasa

Sarkozy arejea kwenye ukumbi wa siasa

Kurejea kwa Nicolas Sarkozy kwenye ukumbi wa siasa nchini Ufaransa huenda ikapelekea kujidhatiti upya kwa chama cha kisoshalisti ambacho kimeonekana kupoteza kwa asilimia kubwa imani kwa wananchi.

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akichukua uamzi wa kurejea kwenye ukumbi wa siasa.
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akichukua uamzi wa kurejea kwenye ukumbi wa siasa. REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wengi kutoka chama cha Kisoshalisti hawafichi tangu wiki iliyopita msimamo wao baada ya kutangazwa kwa Nicola Sarkozy kwenye ukumbi wa siasa. “ Ni miaka miwili sasa tuko pekee madarakani, kwa hiyo tunasubiri jipya analolileta katika siasa za Ufaransa, wamesema wajumbe hao wa chama cha Kisoshalisti.

Kwa upande wake serikali ya Ufaransa, hasa ikulu ya Paris imesema kwamba kurejea kwa Nicolas Sarcozy kwenye ukumbi wa siasa kutaleta kutachangia kuhamasisha mijadala tofauti na ilivyokua hapo awali.

wakati huo huo Julien Dray ametolea wito wafuasi wa chama cha Kisoshalist kudumisha mshikamano kati yao. “ tuwe makini na kuna ulazima tuandae mbinu mpya za kudumisha mshikamano kati yetu, hivi karibuni tutakua na mpizani mkuu”, ametahadhari Dray, ambaye ni mtu wa karibu wa rais wa Ufaransa.

Baadhi ya soshalisti wana imani kwamba rais huyo wa zamani huenda akataka msaada kutoka kwa wafuasi wa mrengo wa kushoto.

Mmoja kati ya mawaziri wa serikali ya Ufaransa, amebaini kwamba muda umepita, huku akikata tamaa kwamba mtu yeyote huenda akashinda uchaguzi. Lakini wadadisi bado wana mashaka ya kurejea kwa Nicolas Sarkozy kwenye ukumbi wa siasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.