Pata taarifa kuu
iran-nyuklia

kiongozi wa kiroho nchini Iran Ayatolah Ali Khomenei aunga mkono mazungumzo ya nchi yake na nchi zenye nguvu

Kiongozi wa kiroho nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei amebaini uungwaji wake mkomno kuhusu mazungumzo juu ya swala la Nyuklia ya Iran yanayoendelea jijini Vienna na mataifa yenye nguvu duniani huku akiweka kando uwezekano wa kusitisha mpango wa Iran wa Urutibishwaji wa madini ya Uranium

Ayatollah Ali Khamenei, Kiongozi wa kiroho nchini Iran
Ayatollah Ali Khamenei, Kiongozi wa kiroho nchini Iran REUTERS/Photo d'archives
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Iran ilikubali kujadiliana na mataifa yaneye nguvu juu ya mpango wake wa Nyuklia unaoshukiwa na mataifa ya magharibi na Israel kuwa unalenga kutengeza zana za Atomiki, Khamenei amesema mazungumzo hayo lazima yaendelee ili kufikia muafaka.

Ujumbe wa Iran pamoja na ule wa mataifa sita yenye nguvu duniani wapo vienna kwa siku ya tatu kuhakikisha mzozo wa Nyuklia wa Iran unakomeshwa. Pande zote mbili katika mazungumzo hayo zimekubaliana kuwa yanaendelea vizuri.

Khamenei amesema katika hotuba yake mbele ya wanayansi wakati wa sherehe za siku ya techologia ya Nyklia licha ya kuendelea kwa mazungumzo hayo, shughuli za urutubishwaji wa Iranium hazitakomeshwa kamwe.

Rais Hassan Rohani aliye chaguliwa Juni 2013, alizunduwa mazungumzo yaliokuwa yamekwamishwa tangu miaka kadhaa. Hata hivyo baadhi ya wajumbe wenye msimamo mkali wamekuwa wakiituhumu serikali kwa kufanya makubaliano kwa faida ya nchi za magharibi.

Makubaliano kati ya nchi sita zenye nguvu yaliofikiwa na Iran, yalianza kutekelezwa tangu januari, huku vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi vikalegezwa, na Iran ikakubali kukaguliwa kwa vinu vyake vya nyuklia, na mazungumzo yanaendelea kuhakikisha muafaka unapatikana ifikapo Julay 20 mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.