Pata taarifa kuu
UFARANSA

Sarkozy arejea nyumbani baada ya kuhojiwa kwa saa 12

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amerejea nyumbani jana jioni baada ya kusikilizwa kwa muda wa saa kumi na mbili mfululuzo na majaji wanaochunguza kesi ya fedha haramu za mwanamama tajiri nchini Ufaransa Ingrid Betancourt. 

Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy,
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, blog.wblakegray.com
Matangazo ya kibiashara

Jaji Jean Michel Gentil na wenzake Cecile Ramanotxo na Valaerie Noel wamemsikiliza rais huyo wa zamani kwa muda mrefu ili kutafuta ushahidi zaidi kuhusu kuhusika kwake katika kesi hiyo ya fedha haramu zilizotolewa na Betancourt katika kufadhili kampeni za uchaguzi wa rais wa mwaka 2007.

kwa mujibu wa wakili wa rais Sarkozy kesi hiyo imesikilizwa katika mazingira yanayokubalika na kuridhishwa na amesema kuridhiswa kuona mteja wake hakuhusishwa katika kashfa hiyo, ingawaje muda wa saa kumi na mbili ni mrefu mno.

Sarkozy amekanusha kuhusika na rushwa ya aina yoyote ile, hata hivyo kama atakutwa na mashtaka atakabiliwa na adhabu kama ilivyokuwa kwa Rais aliyemtangulia Jacques Chirac ambaye alihukumiwa kifungo alipotoka madarakani mwaka 2007 baada ya kukutwa na hatia ya kutokuwa mwaminifu na ubadhirifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.