Pata taarifa kuu
Uturuki

Askari 26 wa Uturuki wauawa na kikundi cha kikurdi

Wanajeshi 26 wa Uturuki wameuawa na waasi wa kikurdi nchini humo katika mashambulio manane tofauti jambo linalo dhihirisha moja kati ya siku mbaya zaidi kwa jeshi tangu kuanza kwa mapigano dhidi ya wapinga umoja nchini humo miaka 27 iliyopita

REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Uturuki limejibu mashambulizi kwa kutumia majeshi ya anga na kwa kupeleka vikosi vyake jirani na Iraq mahali ambako ni ngome ya waasi hao huku waziri mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kiahirisha ziara ya nje ya nchi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuahirisha ziara yake waziri Erdogan amesema kuwa yeyote aneyeunga mkono ugaidi na kujaribu kuwapa hifadhi pamoja na kuwavumilia magaidi anafanya kosa kubwa na kwamba nguvu ya jamhuri ya serikali yake itawashughulikia waliohusika na mashambulio hayo.

Kwa upande wake msemaji wa chama cha PKK Ahmed Denis ameonya kuwa jeshi la Uturuki litashambuliwa vibaya endapo litajaribu kufanya operesheni yoyote ya kijeshi nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Mashambulio hayo nane yaliyofanywa na waasi hao wa chama cha wafanyakazi cha PKK, yametekelezwa katika eneo la Cukurca na Yuksekova katika jimbo la Hakkari jirani na mpaka wa Iraq usiku wa kuamkia leo vyanzo vya usalama nchini humo vimethibitisha.

Idadi ya wanajeshi waliouwawa imedaiwa kuwa kubwa kuwahi kutokea katika jeshi hilo tangu mwaka 1993 wakati ambapo waasi hao waliwaua askari 33 katika jimbo la Bingol Kusini mashariki mwa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.