Pata taarifa kuu
MALI-TIKEN-USANII

Tiken Jah Fakoly alaani jaribio la kumuibia nchini Mali

Mwanamuziki nguli kutoka Cote d'Ivoire Tiken Jah Fakoly anadaikitita cha FCFA milioni 10. Waandalizi wa tamasha la muziki mjini Bamako ndio ambao wanadai, kwa mgogoro ulioanza tangu 2004, miaka 13 iliyopita.

Tiken Jah Fakoly aandaiwa jumla yafedha za Mali (FCFA) milioni 10 (picha ya zamani).
Tiken Jah Fakoly aandaiwa jumla yafedha za Mali (FCFA) milioni 10 (picha ya zamani). RFI / Guillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Tiken Jah Fakoly ambaye aliishi kwa muda mrefu katika mji mkuu wa Mali, Bamako, anaona kuwa ni jaribio la kumuibia.

Mwaka 2004, Tiken Jah Fakoly alikubali kushiriki katika tamasha la kwanza la Muziki wa Bamako, FIMBA. Siku ya tamasha, mwanamuziki huyo hakuweza kufika kwenye ukumbi wa tamasha. Baadaye jioni aliwasili lakini alikataliwa kuingia kwenye ukumbi wa tamasha.

Waandaaji wanalidai fidia ya FCFA milioni 10. Msanii huyo anakataa, kesi hii inaonekana kuwa tete na tayari imeanza kukabiliwa na mambo ya kisiasa. Rais Amadou Toumani Touré ameingilia kati na kufuta kesi hiyo.

Akihojiwa na RFI, Tiken Jah Fakoly amesema: "Nilikuwa nyumbani kwangu, miezi mitatu iliyopita, na kisha nikaambiwa kuwa kuna karani wa mahakama mbele ya mlango wangu. Karani huyu ndiye aliniambia habari hii. Ndio walipokwenda kuona karani mwingine. Karani huyu mpya alileta stabadhi nyumbani kwangu. Nilikuwa safarini,alichunguza nyumba yangu pamoja na askari, ili kuniogopesha! Akaunti zangu za benki zilizuiwa. Waliandikia benki tano kuwa ninadaiwa, na kwamba sheria inawaruhusu kuchukua fedha zangu. Hawa ni watu ambao walitaka tu kuniibia. "

Mwaka 2004, mwanasheria wa waandaaji wa tamasha ni Baber Gano, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mwezi Aprili. Je, uteuzi huu ndio umepelekea walalamikaji kuwa na nguvu zaidi? Waziri amesema kuwa hahusiki katika kesi hiyo na anamuunga mkono msanii kutoka Cote d'Ivoire.

Katibu Mkuu wa FIMBA Adama Kouyaté ambaye alihojiwa a RFI, amesema kuwa kiongozi wa tamasha, Mariam Seye, anataka kupata fedha hiyo ili kulipa mkopo kutoka benki.

Kwa upande wake, Tiken Jah Fakoly anaahidi kuchukua hatua ya kisheria, kwa minajili ya kufuta kabisa kesi hiyo, ambayo anasema inamchafulia jina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.