Pata taarifa kuu
KANISA KATOLIKI-DINI

Makardinali 17 wapya kuteuliwa Vatican

Papa Francis ametangaza Jumapili hii kufanyika mkutano Novemba 19 wa viongozi wa kanisa Katoliki duniani ambapo watatawazwa Makardinali 17 wapya, ikiwa ni pamoja na Waafrika 2, Dieudonné Nzapalainga kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na Maurice Piat kutoka Mauritius.

Askofu Dieudonné Nzapalainga na Imamu mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Oumar Rabin Layama.
Askofu Dieudonné Nzapalainga na Imamu mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Oumar Rabin Layama. AFP
Matangazo ya kibiashara

Askofu Nzapalainga, mwenye umri ulio chini ya miaka 50, ni askofu mkuu mjini Bangui.

Papa Francis alikutana naye wakati wa ziara yake nchini Afrika ya Kati, mwishoni mwa mwaka 2015.

Askofu Piat, yeye anaongoza kanisa Katoliki za Jimbo Kuu la Port-Louis.

Makardinali wapya wanne hawawezi kikao cha Makardinali na kushiriki katika uchaguzi wa kiongozi mpya wa kanisa Katoliki kwa sababu wana umri wa zaidi ya miaka 80.

Makardinali wapyani kutoka mabara 5 na nchi 11.

Wa kwanza kwenye orodha ni Askofu Mario Zenari kutoka Italia, ambaye kwa sasa mwakilishi wa PApa nchini Syria.

Mwezi Februari 2015, Papa Francis aliwateua Makardinali 20 wpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.