Pata taarifa kuu
MAREKANI-MUZIKI-PRINCE

Mwanamuziki Prince amefariki akiwa na umri wa miaka 57

Tovuti ya Marekani ya TMZ imetangaza Alhamisi hii, Aprili 21, kifo cha mwanamuziki Prince. Taarifa hii imethibitishwa na afisa wa mawasiliano ya nyota huyo.

Mwanamuziki Prince wakati wa tamasha lake katika ukumbi wa Stade de France mwezi Juni 2011.
Mwanamuziki Prince wakati wa tamasha lake katika ukumbi wa Stade de France mwezi Juni 2011. AFP/Bertrand Guay
Matangazo ya kibiashara

Prince ambaye alikua akijulikana kwa jina la utani la "The Artis" alifuta tamasha mbili kutokana na matatizo ya kiafya. Mashabiki wake watakumbuka hasa albamu yake ya "1999", iliyomfikisha katika jukwaa la kimataifa.

Prince ambaye alipata umaarufu kwa nyimbo zake kama vile Purple Rain na Kiss alikutwa amekufa katika studio zake za Paisley Park, katika jimbo la Minnesota,tovuti ya TMZ imearifu. Mwanamuziki mashuhuri wa mtindo wa Funk alilazwa hospitalini Ijumaa Aprili 15 kufuatia dalili zinazohusiana na mafua.

"Ni kwa huzuni mkubwa ninathibitisha kwamba mwimbaji mashuhurii, Prince Roger Nelson, amefariki nyumbani katika mji wa Paisley Park asubuhi hii," msemaji wake, Yvette Noel-Schure, amebaini.

Fikra

Prince Roger Nelson alizaliwa mwaka 1958 katika mji wa Minneapolis, na kupewa jina la utani la "mtoto kutoka Minneapolis". Alikuwa mwembambana alikua akipima mita 1.60 za urefu, lakini alikuwa alikua mwanamuziki mashuhuri, mwenye uwezo wa kushawishi pande zote, na kutunga au kuimba nyimbo zote za watu weusi : jazz, funk, hip-hop, soul.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.