Pata taarifa kuu

Ufaransa: Aliyekuwa waziri wa sheria Robert Badinter amefariki

Nairobi – Aliyekuwa waziri wa sheria wa Ufaransa Robert Badinter, aliyesifika kwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita adhabu ya kifo na kuokoa maisha ya watu wengi kwa kujitolea maisha yake katika mapambano dhidi ya adhabu hiyo, amefariki akiwa na umri wa miaka 95.

Aliyekuwa waziri wa sheria wa Ufaransa Robert Badinter amefariki
Aliyekuwa waziri wa sheria wa Ufaransa Robert Badinter amefariki © Bertrand Guay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuteuliwa kama waziri wa sheria katika serikali ya Kisoshalisti ya Rais Francois Mitterrand, mwezi Juni mwaka 1981, Badinter, alifanya suala la kukomesha adhabu ya kifo kuwa kipaumbele chake cha kwanza.

Hata hivyo, harakati zake zilibadilika na kuchukua sura mpya mwaka 1972 baada ya mmoja wa wateja wake, Roger Bontems, kukatwa kichwa baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya muuguzi na mlinzi wakati alipojaribu kutoroka gerezani.

Wakili huyo ambaye alisema hawezi kufuata "mfumo wa utoaji haki kwa kuua", alijikuta akikashifiwa n ahata kutukanwa kwa kujaribu kusukuma sheria inayopiga marufuku hukumu ya kifo wakati ambapo Wafaransa wengi bado wanaiunga mkono.

Badinter, Alizaliwa jijini Paris Machi 30, 1928 na mfanyabiashara wa Kiyahudi Myahudi ambaye alikuwa amehamia kutoka Bessarabia, ambayo sasa ni Moldova na alipokuwa na miaka 14 baba yake alikuwa miongoni mwa kundi la Wayahudi waliotolewa kusini-mashariki mwa Lyon na kuhamishwa katika kambik ya mateso ya Sobibor nchini Poland wakati wa utawala wa Kinazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.