Pata taarifa kuu
SHERIA-MAANDAMANO

Watu 150,000 waingia mitaani nchini Ufaransa kupinga sheria ya uhamiaji

Watu 150,000 wameshiriki kote Ufaransa katika maandamano yaliyoandaliwa Jumapili Januari 21 dhidi ya sheria ya uhamiaji, ikiwa ni pamoja na 25,000 huko Paris, amesema katibu mkuu wa shirikisho kuu la wafanyakazi ,CGT, Sophie Binet kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Maandamano ya wanaopinga sheria ya uhamiaji nchini Ufaransa huko Paris, Jumapili, Jan. 21, 2024. Mahakama ya Katiba inapitia upya sheria ya uhamiaji yenye utata wiki ijayo.
Maandamano ya wanaopinga sheria ya uhamiaji nchini Ufaransa huko Paris, Jumapili, Jan. 21, 2024. Mahakama ya Katiba inapitia upya sheria ya uhamiaji yenye utata wiki ijayo. AP - Thomas Padilla
Matangazo ya kibiashara

Β 

Maelfu kadhaa ya wapinzani wa sheria ya uhamiaji wameandamana katika miji ya Paris, Bordeaux, Toulouse, Lille na kwingineko nchini Ufaransa siku ya Jumapili Januari 21 kudumisha shinikizo dhidi ya kupitishwa kwa nakala ambayo, kulingana na waandamanaji hao, yanaweka ushindi wa kiitikadi "wa mrengo wa kulia" kabla ya uamuzi wa Baraza la Katiba mnamo Januari 25.

Makao makuu ya polisi ya Paris yamehesabu waandamanaji 16,000 katika maandamano ya Paris, ambayo ni makubwa zaidi kati ya maandamano 160 yaliyopangwa kufanyika Jumapili nchini Ufaransa, ili kujibu wito uliyozinduliwa awali na watu 201 dhidi ya nakala hii tata.

Kwa kuunga mkono wito uliozinduliwa hapo awali na viongozi 201, wapinzani wanataka kuhamasisha waanchi kuweka shinikizo kwa serikali, ambayo inaweza kutangaza haraka nkala hii iliyopigiwa kura katikati ya mwezi Desemba mwaka uliyopita

Waandamanaji wapatao 75,000, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani, 150,000 kulingana na CGT, walikusanyika kote Ufaransa kwa wito uliozinduliwa hapo awali na viongozi 201.

Zaidi ya maandamano 160 yalipangwa kote Ufaransa. Kati ya waandamanaji 3,000 na 4,000 kulingana na waandalizi, waliandamana katika mitaa ya Toulouse siku ya Jumamosi. Mamia ya watu walikusanyika huko Metz Jumapili asubuhi. Huko Caen, vyama vya wafanyakazi vilidai kati ya waandamanaji 1,500 na 2,000 Jumapili asubuhi.

Huko Lille, karibu watu 2,000 wameandamana, wakiongozwa na wafanyakazi kutoka jamii za EmmaΓΌs du Nord, ambao wamekuwa kwenye mgomo kwa miezi sita kushutumu mazingira yao ya kazi na kudai kuratibiwa kwao.

"Sheria hii ni kuvunja kanuni za Ufaransa tangu 1789 kwa haki za ardhi na tangu 1945 kwa ulinzi wa kijamii kwa wote," amesema katibu mkuu wa CGT, Sophie Binet, ambaye akishirikiana na mwenzake wa CFDT, Marylise LΓ©on, wametoa wito wa kufanyika kwa mandamano kote nchini kupinga sheria hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.