Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa anazuru Kyiv
Nairobi – Waziri mpya wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne yuko jijini Kyiv, hii ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasimi nje ya nchi.
Imechapishwa:
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hatua hii ni njia moja ya Ufaransa kuonyesha kuendelea kusimama na Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Ziara yake inkuja wakati huu washirika wa Kyiv wakiendelea kutafuta njia za kuendelea kusimama na Ukraine, suala la ufadhili likipewa kipau mbele.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X, zamani ukijulikana kama Twitter na wizara yake, Stephane Sejourne aliwasili Kiev kwa ziara yake ya tangu kuteuliwa kwa nafasi hiyo kuendeleza juhudi za kidiplomasia za Ufaransa huko na kusisitiza kujitolea kwa Ufaransa kwa washirika wake na kwa raia wa Ukraine.
🇺🇦🇫🇷🇪🇺Depuis près de 2 ans, l’Ukraine est en première ligne pour défendre sa souveraineté et assurer la sécurité de l’Europe.
— Stéphane Séjourné (@steph_sejourne) January 13, 2024
L’aide de la France s’inscrit dans la durée.
C’est ce que je suis venu dire à Kiev pour mon premier déplacement. pic.twitter.com/xyAlKyKPs3
Sejourne, ambaye alichukua nafasi ya Catherine Colonna katika mabadiliko ya serikali siku ya Alhamisi, anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Sejourne, 38, ambaye tofauti na Colonna hana historia ya kuwa mwanadiplomasia kitaaluma, ni mshirika wa karibu wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na katibu mkuu wa chama cha rais cha Renaissance.
Tayari alikuwa ameahidi kuendelea kuunga mkono Ukraine, ambayo imekuwa imekuwa vitani na nchi ya Urusi kwa karibu miaka miwili, alipochukua rasmi madaraka Ijumaa.
Msaada wa kijeshi wa Ufaransa kwa Ukraine ni sawa na euro bilioni 3.2 (dola bilioni 3.5), kulingana na ripoti ya bunge iliyochapishwa mnamo Novemba.
Rais Zelensky alionya kuwa ucheleweshaji wowote wa misaada unaweza kuathiri vibaya mwenendo wa vita.
Pia amesisitiza kuwepo kwa ulinzi zaidi wa anga, kwani nchi yake imekuwa ikikabiliwa na mashambulio mapya ya angani kutoka Urusi.
Haya yanajiri wakati huu Urusi ikirusha makombora 40 na ndege zisizo na rubani nchini Ukraine usiku kucha.