Pata taarifa kuu

Ufaransa;Brigitte Macron anaitembelea familia ya kijana aliyejiua Poissy, magharibi mwa Paris

Nairobi – Mke wa rais wa Ufaransa Brigitte Macron, atatembelea familia ya kijana aliyejiua baada ya kudhulumiwa shuleni katika eneo la Poissy,lililoko magharibi mwa Paris.Hii ikiwa ni moja wapo ya maswala muhimu anayoshughulikia mke huyo wa Rais.

Mke wa Rais wa Ufaransa,Brigitte Macron ataitembelea familia ya kijana aliyejitia uhai baada ya kudhulumiwa shuleni
Mke wa Rais wa Ufaransa,Brigitte Macron ataitembelea familia ya kijana aliyejitia uhai baada ya kudhulumiwa shuleni © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Ni hisia zinazotuzidia  sisi sote wakati mtoto wa umri wa miaka 15 hawezi kuona suluhisho lolote zaidi ya kujiua," msemaji wa serikali Olivier Veran aliambia shirika la habari  la France Inter.

Waendesha mashtaka wa Versailles wanachunguza kifo cha Jumanne cha kijana huyo huko Poissy, magharibi mwa Paris, wakiambia AFP kwamba wanakuwa makini sana  kuhusu sababu za kifo chake.

Alikuwa ameripoti kudhulumiwa mnamo Desemba mwaka jana, huku wazazi wake wakilalamika kwamba kesi hiyo haikushughulikiwa vya kutosha na shule yake, alisema waziri wa Elimu Gabriel Attal.

Mke wa Macron na ambae pia amewahi kuwa mwalimu, anavichukulia na uzito sana visa kama hivi na vile vya uonevu mitandaoni.

Takriban mtoto mmoja kati ya 10 wa shule katika nchi hiyo ya  Ufaransa wanaaminika kuteseka kutokana na uonevu, jambo ambalo liliibua orodha ya vipaumbele vya serikali baada ya kujiua kwa msichana wa miaka 13 kaskazini mwa Ufaransa mapema mwaka huu.

 "Uonevu shuleni ni janga. Mamia ya maelfu ya vijana ni wahasiriwa... hatuwezi kupuuza chochote hata kidogo, hatuwezi kufikiria kuwa hii ni hali mbaya ya watoto," Waziri Mkuu Elisabeth Borne. alisema Jumapili.

 Masharti mapya ya mwaka wa shule wa 2023-24 ni pamoja na mabadiliko yanayomaanisha kuwa wahusika wa unyanyasaji wanaweza kuhamishwa hadi shule tofauti, badala ya kuwalazimisha waathiriwa kuhama.

Kila shule itakuwa na mfanyakazi anayehusika na kupambana na unyanyasaji, waziri Attal alisema, akiongeza kwamba watahitajika pia "kiutaratibu" kupeleka kesi kwa waendesha mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.