Pata taarifa kuu

Ukraine: Zelensky amteua Roustem Oumerov kuwa Waziri mpya wa Ulinzi

Roustem Oumerov atakuwa Waziri mpya wa Ulinzi, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza Jumapili usiku. Anachukua nafasi ya Oleksiï Reznikov. Roustem Umerov ni kiongozi mashuhuri wa jumuiya ya Kitatari ya Crimea ambaye aliwakilisha Kyiv katika mazungumzo nyeti na Moscow.

Wanajeshi wa Ukraine, wakiwa katika operesheni katika mkoa wa Luhansk, Juni 8, 2023.
Wanajeshi wa Ukraine, wakiwa katika operesheni katika mkoa wa Luhansk, Juni 8, 2023. © AP/Roman Chop
Matangazo ya kibiashara

Bw. Umerov, 41, alizaliwa katika jamhuri ya zamani ya Soviet ya Uzbekistan, ambapo familia yake ilikimbilia uhamishoni chini ya utawala wa Stalin, na alikuwa mtoto wakati familia yake ilipohamia Crimea wakati Watatari waliruhusiwa kurudi, katika miaka ya 80 na miaka ya 90. Alianzia katika tasnia ya mawasiliano mnamo 2004, na ni mbunge tangu mwaka 2019.

Katika Bunge, alikuwa mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Crimea, ambalo liliratibu juhudi za kidiplomasia za kimataifa za kufuta hatua ya Urusi ya unyakuzi wajimbo hilo la Crimea mwaka 2014. Kwa miaka mingi alikuwa mshauri wa kiongozi wa kihistoria wa Tatari ya Crimea, Mustafa Dzhemilev.

Urusi iliidhinisha unyakuzi wake wa Crimea kwa kura ya maoni iliyochukuliwa kuwa kinyume cha sheria na Ukraine na washirika wake wa Magharibi. Watatari, ambao wanajumuisha 12% hadi 15% ya wakazi wa Crimea, kwa kiasi kikubwa walisusia kura hii ya maoni. Kwa sababu hiyo, Moscow iliharamisha Mejlis, kusanyiko la kitamaduni la Waislamu wachache wa Kitatari, na kulitaja kuwa kundi lenye msimamo mkali, ambalo wanachama wengi walifungwa gerezani.

Baada ya kunyakuliwa kwa Crimea na vile vile baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022, Roustem Oumerov ameshiriki mara kadhaa katika mazungumzo ya siri na Moscow, hasa juu ya kubadilishana wafungwa na uhamishaji wa raia. Alikuwa sehemu ya wajumbe wa Ukraine kwenye mazungumzo na Moscow, chini ya uangalizi wa Uturuki na Umoja wa Mataifa, ambayo yaliwezesha kuanzishwa kwa eno salama la baharini kuruhusu usafiri wa nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi. Makubaliano ambayo Urusi ilijiondoa hivi karibuni.

Kupambana na rushwa katika jeshi

Mnamo Septemba 2022 Bw. Oumerov aliteuliwa kuwa mkuu wa Hazina ya Mali ya Serikali, nafasi ya juu katika nchi ambayo mchakato wa ubinafsishaji umejaa ufisadi. Wizara ya Ulinzi aliyoachiwa na mtangulizi wake Oleksiï Reznikov pia imetajwa katika kashfa za ufisadi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza mnamo Agosti 11 kuwafuta kazi maafisa wote wa kikanda wanaohusika na kuajiri wanajeshi wapya ili kukomesha mfumo wa rushwa unaowaruhusu askari kutoroka jeshi.

Akitangaza kwamba anataka kumfanya waziri wake mpya wa ulinzi, Bw. Zelensky amebaini kwamba atawasilisha uteuzi wake kwa Bunge wiki hii. "Bunge linamfahamu mtu huyu vyema na Bw. Umerov haitaji utambulisho wowote wa ziada," aameongeza rais wa Ukraine.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.