Pata taarifa kuu

Urusi: Rais Putin awataka wapiganaji wote kula kiapo

Nairobi – Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amewagiza mamluki wote wa kundi la Wagner na wapiganji wengine nchini humo kula kiapo cha kuetetea na kutii serikali ya Kremlin.

Agizo la Putin linafuatia lile la wizara ya ulinzi ya Urusi, mwezi juni kutaka wapiganji wa Wagner kusaini mkataba wa kijeshi
Agizo la Putin linafuatia lile la wizara ya ulinzi ya Urusi, mwezi juni kutaka wapiganji wa Wagner kusaini mkataba wa kijeshi REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa taarifa ya Putin ni kwamba agizo hilo linastahili kuheshimiwa na raia wote wa Ukraine ambao wanahusika kwa ulinzi wa taifa la Urusi.

Ni agizo linalokuja siku chache baada ya kiongozi wa Kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ambaye aliongoza uasi kwa muda mfupi mwezi Juni, kudaiwa kufariki kupitia ajali ya ndege.

Agizo la Putin linafuatia lile la wizara ya ulinzi ya Urusi, mwezi juni kutaka wapiganji wa Wagner kusaini mkataba wa kijeshi, ambapo Yevgeny alisusia kusaini mkataba huo akisema hakutaka wapiganaji wake kuwekwa chini ya wizara.

Haya yanajiri wakati huu Moscow ikiendelea kukanusha kuhusika na kifo cha Yevgeny, ambapo watu wengine 9 pia walifariki kutokana na ajali hiyo ya ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.