Pata taarifa kuu

Lukashenko: Nilimuonya Prigozhin kuhusu vitendo vyake

Rais wa Belarus Alexander  Lukashenko amesema kuwa aliwaonya wakuu wa mamluki wa Wagner wa Urusi Yevgeny Prigozhin na Dmitry Utkin wawe makini sana na kusisitiza kuwa wapiganaji wa Wagner watasalia Belarus kufuatia madai ya kufariki kwa viongozi wa kundi hilo.

Rais wa Belarus Alexander  Lukashenko amesema kuwa aliwaonya wakuu wa mamluki wa Wagner wa Urusi Yevgeny Prigozhin na Dmitry Utkin wawe makini sana
Rais wa Belarus Alexander  Lukashenko amesema kuwa aliwaonya wakuu wa mamluki wa Wagner wa Urusi Yevgeny Prigozhin na Dmitry Utkin wawe makini sana © Stringer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Lukashenko, ambaye alisaidia upatikanaji wa  makubaliano ambayo yalipelekea wapiganaji wa Wagner kuingia nchini Belarus kwa amani kufuatia uasi wao uliozuiliwa mwezi Juni, alisema wakati huo kwamba alikuwa amemshawishi Putin "kutomuua" Prigozhin.

Akizungumzia kuhusu madai ya kifo cha Prigozhin katika ajali ya ndege nchini Urusi wiki hii, Lukashenko alisema Ijumaa kwamba kiongozi huyo wa Wagner alitupilia mbali mara mbili wasiwasi uliotolewa kuhusu hatari ambayo ilionekana wazi kuwa ingesababisha kifo chake.

Inadaiwa kuwa mkuu huyo wa Wagner aliuawa katika ajali hiyo ndege
Inadaiwa kuwa mkuu huyo wa Wagner aliuawa katika ajali hiyo ndege REUTERS - STRINGER

Mkuu wa huyo wa Belarus alisema kwamba wakati wa uasi huo, alikuwa ameonya Prigozhin kwamba "atakufa" ikiwa ataendelea kuandamana kwenda Moscow, suala ambalo alisema Prigozhin alipuuza.

Lukashenko, ambaye ni mtu wa karibu wa Prigozhin na rais Putin, ameendelea kusisitiza kwamba kifo cha mkuu huo Wagner hakikusababishwa na Putin.

Utawala wa Kremlin umetupilia mbali madai ya mataifa ya Magharibi kuwa ulihusika na kifo cha mkuu wa Wagner
Utawala wa Kremlin umetupilia mbali madai ya mataifa ya Magharibi kuwa ulihusika na kifo cha mkuu wa Wagner REUTERS - MAXIM SHEMETOV

Siku ya Ijumaa, utawala wa Kremlin ulitupilia mbali madai ya mataifa ya Magharibi kwamba Prigozhin aliuawa kwa maelekezo ya uongozi wa Urusi.

Moscow inasema tuhuma hizo na Magharibi ni za uongo na kwamba kunahitajika kuwepo kwa subira kubaini chanzo na kifo cha mkuu huyo wa Wagner.

Rais wa Belarus anasema wapuganaji hao watasalia nchini mwake
Rais wa Belarus anasema wapuganaji hao watasalia nchini mwake © REUTERS/Anastasia Barashkova

Licha ya hayo, rais Lukashenko amesisitiza kuwa wapiganaji wa Wagner watasalia nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.