Pata taarifa kuu

Élysée yarasimisha mabadiliko madogo ya serikali

Baada ya mazungumzo marefu kati ya Emmanuel Macron na waziri wake mkuu Elisabeth Borne, Élysée imetangaza siku ya Alhamisi alaasiri kumalizika kwa "marekebisho" ya baraza la mawaziri. Vyanzo vya habari ndani ya wengi vimetoa majina ya wajumbe wapya wa serikali hata kabla ya tangazo rasmi.

Gabriel Attal, ambaye kwa sasa ni Waziri Mjumbe wa Bajeti, anachukua nafasi ya Pap Ndiaye kkama waziri wa Elimu.
Gabriel Attal, ambaye kwa sasa ni Waziri Mjumbe wa Bajeti, anachukua nafasi ya Pap Ndiaye kkama waziri wa Elimu. AFP - BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Mara ya kwanza ikitarajiwa Jumatano, mabadiliko haya yamekuwa yakizunguka kambi ya rais kwa wiki kadhaa. Élysée imekamilisha rasmi mashauriano kuhusiana na wajumbe wapya wa serikali. Mwanzoni mwa mwaka wa shule, serikali hii mpya italazimika kukabiliana na changamoto zilizowekwa na rais kuhusu ikolojia, uhamiaji na kukabiliana na ghasia zilizofuatia kifo cha Nahel, huko Nanterre, katika vitongoji vya Paris.

Waziri wa Elimu, Pap Ndiaye, ameondolewa kwenye nafaisi yake kama waziri wa Elimu. Nafasi yake imechukuliwa naGabriel Attal, 34, vyanzo kadhaa vya wengi kutoka kambi ya rais vimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi. Wakati huo huo Mbunge wa chama cha Renaissance Thomas Cazenave ameteuliwa kuwa Waziri wa Hesabu za Umma.

Kwa upande wake, Aurélien Rousseau, mkurugenzi wa zamani katika ofisi ya Élisabeth Borne huko Matignon, atateuliwa kuwa Waziri wa Afya akichukua nafasi ya daktari François Braun, kulingana na shirika la habari la AFP, likinukuu vyanzo vinavyojua suala hilo, likithibitisha habari kutoka kwa kituo cha BFMTV.

Mabadiliko ya wakuu wa wizara hizi mbili muhimu, kuhusu masuala ya kipaumbele kwa muhula wa pili wa miaka mitano wa Emmanuel Macron, yanaonekana kuashiria kwamba Waziri Mkuu, Élisabeth Borne, amefanikiwa kwa kiasi fulani katika dau lake. Mawaziri na washauri walikuwa wakielezea tangu Jumatatu vita vya kimya kimya kati ya mkuu wa serikali, ambaye alitarajia kufanya upya angalau nyadhifa hizi mbili ili kuweka mamlaka yake, na Rais wa Jamhuri ambaye alitaka tu mabadiliko nafasi za kawaida.

Aurore Bergé katika Wizara ya Mshikamano

Majina mengine yaliyotolewa kabla ya tangazo rasmi, linatajwa jina la kiongozi wa wa kundi la wabunge wa chama cha Renaissance katika Bunge, Aurore Bergé. Atachukua nafasi ya Jean-Christophe Combe mkuu wa Wizara ya Mshikamano, pia vyanzo vya kutoka kwa wengi vimeliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.