Pata taarifa kuu

Urusi imeonya kuhusu hatua ya kuihami Ukraine na ndege za kivita F-16

Urusi itachukulia ndege za kivita za Magharibi za F-16 zinazotumwa Ukraine kama tishio la "nyuklia" kwa sababu ya uwezo wake wa kubeba silaha za atomiki, Waziri wa mambo ya nje nchini humo Sergei Lavrov amesema.

Ndege aina ya F-16 ya Uholanzi
Ndege aina ya F-16 ya Uholanzi © 路透社图片
Matangazo ya kibiashara

Kyiv imekuwa ikitoa wito kwa washirika wake nchi za Magharibi kuipa ndege za kivita za kisasa haswa wakati huu inapopambana dhidi ya mashambulio ya Urusi.

Lavrov amezungumzia kuhusu mpango wa Marekani wa kuipa Kyiv ndege za kivita aina ya F-16, ingawa Washington haijatoa idhini kwa nchi yoyote kuzisambaza.

"Urusi haiwezi kupuuza uwezo wa ndege hizi kubeba silaha za nyuklia. Hakuna uhakikisho wowote utasaidia hapa," Lavrov alinukuliwa akisema na wizara ya mambo ya nje ya Urusi.

Uholanzi na Denmark zinaongoza mpango wa kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kuhusu kutumia ndege hiyo iliyotengenezwa nchini  Marekani kama sehemu ya muungano wa mataifa 11.

Mpango huo utaanza nchini Denmark mwezi Agosti baada ya Marekani kuidhinisha hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.