Pata taarifa kuu

Watu nane wameuawa katika shambulio la Urusi mashariki mwa Ukraine

Nairobi – Watu nane wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa katika eneo la Lyman mashariki mwa Ukraine baada ya mji huo kushambuliwa kwa roketi ya Urusi, wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema.

Mapigano nchini Ukraine yameingia katika siku yake ya 500
Mapigano nchini Ukraine yameingia katika siku yake ya 500 REUTERS - RFE/RL/SERHII NUZHNENKO
Matangazo ya kibiashara

"Kufikia sasa tunajua takriban watu 8 waliofariki... Idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka hadi watu 13," wizara hiyo imesema kwenye mtandao wa kijamii.

Jengo la makazi jirani na  nyumba ya uchapishaji na magari matatu yaliharibiwa katika shambulio hilo, ilisema.

Lyman, kituo kikuu cha reli, hapo awali kilikuwa kinadhibitiwa na vikosi vya Urusi lakini kikachukuliwa tena na jeshi la Ukraine mnamo Oktoba.Ukraine imeripoti operesheni za mashambulio ya Urusi katika eneo hilo wiki hii.

Katika mji unaodhibitiwa na Urusi wa Oleshky kusini mwa Ukraine, afisa wa huduma za dharura alinukuliwa na shirika la habari la TASS akisema raia wawili waliuawa katika mashambulio ya Ukraine usiku kucha.

Vikosi vya Ukraine mwezi uliopita vilianza mashambulio ya kurudisha eneo linalodhibitiwa na Urusi mashariki na kusini mwa nchi hiyo.

Wakikabiliana na safu zenye nguvu za ulinzi za Urusi, wameteka tena mamia ya kilomita za mraba na karibu na vijiji kadhaa baada ya zaidi ya mwezi mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.