Pata taarifa kuu
HAKI-USALAMA

Ufaransa: Mamia wakusanyika Paris kwa kumkumbuka Adama Traoré, licha ya marufuku

Mandamano ya kila mwaka ya kumbukumbu ya Adama Traoré, aliyeuawa wakati wa alipokamatwa na maafisa wa usalama mwaka 2016, ulipigwa marufuku na makao makuu ya polisi ya Paris Jumamosi hii. Wito wa kukusanyika katika eneo la Jamhuri "Place de la République" Jumamosi hii Julai 8 huko Paris ulitolewa kwenye mitandao ya kijamii na kundi linalotetea haki kwa Adama Traoré.

Mwanaharakati wa Ufaransa Assa Traoré anazungumza mbele umati wa watu, katika eneo la Place de la République, mjini Paris mnamo Julai 8, 2023, miaka saba baada ya kaka yake Adama Traoré kufariki akiwa mikononi mwa polisi.
Mwanaharakati wa Ufaransa Assa Traoré anazungumza mbele umati wa watu, katika eneo la Place de la République, mjini Paris mnamo Julai 8, 2023, miaka saba baada ya kaka yake Adama Traoré kufariki akiwa mikononi mwa polisi. © Bertrand Guay, AFP
Matangazo ya kibiashara

Saa tisa alaasiri, eneo la Jamhuri "Place de la République" huko Paris lilikuwa tulivu. Kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP, angalau watu 2,000 walishiriki maandamano hayo. Kumeonekana idadi kubwa ya maafisa wa polisi, magari ya polisi, hasa, yakiwa yaliegeshwa karibu na Place de la République. Polisi kimsingi hufanya ukaguzi wa utambulisho kwa watu waliopo kwenye uwanja huo. Kulikuwa na watu wachache kwa wakati huo, karibu watu hamsini zaidi, pia viongozi wa vyama walikuwepo. Jean-Claude Samouiller, mkuu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International nchini Ufaransa, amekuwepo.

Assa Traoré, dada wa Adama Traoré na mtu mashuhuri katika vita dhidi ya ghasia za polisi, alitangaza kwamba atakuwepo "Jumamosi saa tisa alaasiri Place de la République", baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano yaliyopangwa huko Persan na Beaumont-sur-Oise, katika eneo la Val-d'Oise, kwa kumbukumbu ya kaka yake aliyefariki muda mfupi baada ya kukamatwa na maafisa wa polisi mnamo mwezi Julai 2016.

Mahakama katika uamuzi wake ilisema kuwa iwapo maandamano hayo yataendelea huenda yakazua machafuko wakati huu hofu ikiwa ingalipo kufuatia kuawaua kwa Nahel kijana mwenye umri wa miaka 17 raia wa Algeria na afisa wa polisi.

Kupitia ujumbe wa video uliochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa Assa Traore, dada mkubwa wa Adama Traore, alithibitisha kwamba kutokana na uamuzi wa mahakama maandamano hayatafanyika katika eneo la Beaumont-sur-Oise".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.