Pata taarifa kuu

Maandamano dhidi ya polisi yamepangwa kufanyika nchini Ufaransa

Maandamano zaidi yanatarajiwa kushuhudiwa nchini Ufaransa dhidi ya kile kinachodaiwa na matumizi ya nguvu kupita zaidi ya maofisa polisi hatua inayokuja baada ya mamlaka kupiga mafaruku mkutano wa kumbukumbu kwa hofu kuwa hatua hiyo inaweza kuwa mwendelezo wa machafuko ya awali.

Dada ya Adama Traoré, Assa, wakati wa maandamano ya kumkumbuka kijana huyo huko Paris, Julai 30, 2016.
Dada ya Adama Traoré, Assa, wakati wa maandamano ya kumkumbuka kijana huyo huko Paris, Julai 30, 2016. DOMINIQUE FAGET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka saba baada ya kijana mweusi Adama Traore, kufariki akiwa mikononi mwa polisi, dada yake alikuwa amepanga kuongoza maandamano ya kumkumbuka kaskazini mwa Paris.

Mahakama katika uamuzi wake ilisema kuwa iwapo maandamano hayo yataendelea huenda yakazua machafuko wakati huu hofu ikiwa ingalipo kufuatia kuawaua kwa Nahel kijana mwenye umri wa miaka 17 raia wa Algeria na afisa wa polisi.

Kupitia ujumbe wa video uliochapishwa kwenye ukurasa wa twitter wa Assa Traore, dada mkubwa wa Adama Traore, alithibitisha kwamba kutokana na uamuzi wa mahakama maandamano hayatafanyika katika eneo la Beaumont-sur-Oise".

"Serikali imeamua kuongeza mafuta kwa moto na kukosa kuheshimu kifo cha kaka yangu” alisema kupitia ujumbe wa video.

Maandamano  dhidi ya ghasia za polisi yamepangwa kote nchini Ufaransa wikendi hii, ikijumuisha katika miji ya Lille, Marseille, Nantes na Strasbourg. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.