Pata taarifa kuu

Ukraine: Watu wanne wameuawa katika shambulio la Urusi

Nairobi – Urusi imetekeleza shambulio kwenye majengo ya makazi katika mji wa Lviv nchini Ukraine ambapo watu wanne wamethibitishwa kuawaua katika shambulio ambalo gavana wa mji huo amelitaja kuwa kubwa zaidi kuwahi tekelezwa katika maeneo ya makazi ya raia tangu Moscow kuishambulia Kyiv.

Watu wanne wameuawa katika shambulio ambalo limetekelezwa na Urusi
Watu wanne wameuawa katika shambulio ambalo limetekelezwa na Urusi © AP / Mykola Tys
Matangazo ya kibiashara

Licha ya Urusi kutekeleza mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani nchini Ukraine, Mji wa Lviv unaopatikana Magharibi mwa taifa hilo karibu na mpaka wa Poland, haujakuwa ikiripoti mashambulio.

Kwa mujibu wa maofisa wa uokoaji, shughuli za kuwatafuta watu wanaodhaniwa kukwama chini ya vifusi vya jengo hilo inaendelea.

Shughuli za ukozi inaendelea kwa mujibu wa mamlaka katika eneo hilo
Shughuli za ukozi inaendelea kwa mujibu wa mamlaka katika eneo hilo © REUTERS / ROMAN BALUK

Picha zilizonaswa kutoka kwenye eneo la tukio, maofisa hao wameonekana wakiendelea na shughuli hiyo wakati magari yaliokuwa kando ya jengo hilo yakionekana yakiwa yameharibiwa vibaya.

Andriy Sadovyi meya wa mji huo kupitia ukurasa wake wa Telegram ameeleza kwamba zaidi ya majengo 50 yameribiwa yakiwemo yale ya chuo cha ufundi cha Lviv.

Inadaiwa kuwa huenda baadhi ya watu wakawa wamenaswa chini ya vifusi
Inadaiwa kuwa huenda baadhi ya watu wakawa wamenaswa chini ya vifusi © ДСНС України

Naye rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika kuwa “haya ndiyo madhara ya shambulio la usiku ambalo limetekelezwa na Urusi” akichapisha video inayoonyesha uharibifu wa majengo.

Haijawekwa wazi ni makombora mangapi yaliorushwa katika majengo hayo na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.