Pata taarifa kuu

Ufaransa inasema maandamano dhidi ya polisi yamepungua

Nairobi – Wizara ya usalama nchini Ufaransa imesema kasi ya machafuko na maandamano yaliokuwa yakishuhudiwa katika baadhi ya miji imepungua katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Mamea nchini Ufaransa wametoa wito wa kuwepo kwa utulivu
Mamea nchini Ufaransa wametoa wito wa kuwepo kwa utulivu REUTERS - NACHO DOCE
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii inakuja baada ya maandamano makubwa yenye ghasia kushuhudiwa katika baadhi ya miji nchini Ufaransa kulalamikia mauaji ya kijana mwenye umri wa miaka 17 na afisa wa polisi.

Watu 72 wameripotiwa kukamatwa katika oparesheni ya polisi nchi nzima wakiwemo 24 jijini Paris na maeneo jirani ambapo pia majengo 24 yameripotiwa kuchomwa moto.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa magari 159 yameteketezwa, mapipa 202 yakusanya taka yakichomwa moto katika maeneo ya umma.

Mamea nchini humo wametoa wito wa kuwepo kwa utulivu
Mamea nchini humo wametoa wito wa kuwepo kwa utulivu © EMMANUEL DUNAND / AFP

Maofisa wanne wa polisi na wazima moto wameripotiwa kushambuliwa japokuwa hawakujeruhiwa.

Licha ya kuripotiwa kupungua kwa kasi ya maandamano, idadi  imesalia kuwa kawaida ya polisi 45,000 katika maeneo yote nchini Ufaransa.

Serikali ya Ufaransa imekuwa ikikabiliana na waandamanaji na uporaji wa mali tangu kuawaua kwa Nahel M. kijana mwenye umri wa miaka 17 na afisa wa polisi katika eneo la trafiki Jumanne iliyopita.

Baadhi ya waandamanaji wameripotiwa kukamatwa na polisi
Baadhi ya waandamanaji wameripotiwa kukamatwa na polisi AP - Jean-Francois Badias

Kitendo hicho cha afisa huyo, kimeibua hasira na ghadhabu kuhusu madai ya maofisa kuhusika na vitendo vya kibaguzi.

Mameya nchini humo wamefanya mkutano siku ya Jumatatu kutoa wito wa kumalizika kwa machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.