Pata taarifa kuu

Ufaransa: Bibi ya kijana aliyepigwa risasi na polisi atoa wito wa utulivu

Nairobi – Nchini Ufaransa, nyanya au bibi wa mvulana mwenye umri wa miaka 17, aliyepigwa risasi na polisi na kuzua makabiliano makali katika miji ya nchi hiyo kukalamikia mauaji hayo, ametoa wito wa utulivu na kuwataka waandamanaji kuacha kufanya uharibifu kama kuchoma magari.

Ghasia zimeanza kupungua katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa polisi
Ghasia zimeanza kupungua katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa polisi AFP - CLEMENT MAHOUDEAU
Matangazo ya kibiashara

Machafuko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali katika baadhi ya miji nchini humo, maduka yakiporwa, magari yakichomwa moto na miundo mbinu nyengine kuharibiwa vibaya.

Akizungumza na Televisheni ya BFM, Nadia, ambaye ni nyaya au bibi yake Nahel aliyeuawa, amewashtumu waandamanaji kutumia kifo cha mjukuu wake kama kisingizio cha kufanya uharibifu.

β€œNamtaka polisi aliyemuua mjuku wangu, huyu ndiye ninayemtaka, uzuri ni kwamba maofisa wa polisi wamejitokeza wengi lakini sasa hao wanaoendelea kuvunja majumba na wasihi sana acheni. ” alisema bibi yake Nahel aliyeuawa.

00:39

Bibi yake Nahel aliyeuawa

Ametoa wito huu baada ya waandamanaji kuvamia makaazi ya Meya, wa mji ulio nje ya jiji la Paris na kuteketeza moto gari lake.

Rais Emmanuel Macron siku ya Jumanne, anatarajiwa kukutana na Mameya wa miji inayoshuhudia machafuko hayo yaliyosababisha uharibifu mkubwa.

Haya yanajiri wakati huu ambapo vyombo vya usalama nchini humo vikiripoti kukamatwa kwa waandamanaji 157 usiku wa kuamkia leo, hatua inayokuja wakati huu ambapo kasi ya maandamano hayo yenye vurugu ikiaanza kupungua.

Maofisa wa polisi ni miongoni mwa waliojeruhuiwa katika maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.