Pata taarifa kuu

Rais Putin ameishtumu Ukraine na washirika wake kwa kutaka Warusi wauane

Nairobi – Rais wa Urusi Vladimir Putin, ameishtumu Ukraine na washirika wake, mataifa ya Magharibi kwa kutaka Warusi wauane, kufuatia jaribio la kundi la mamluki la Wagner kutaka kulipindua jeshi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais wa Urusi Vladmir Putin amefanya kikao cha dharura na wakuu wa usalama nchini humo
Rais wa Urusi Vladmir Putin amefanya kikao cha dharura na wakuu wa usalama nchini humo via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa mara ya kwanza, baada ya Wagner kusitisha mpango yake na kurejea kwenye kambi zao, Putin amesema alitoa maagizo, kuhakikisha kuwa hakuna umwagaji wa damu unaotokea na kutoa msamaha  kwa mamluki hao, ambao walitishia uongozi wake.

Putin ameitaja Ukraine na mataifa ya Magahribi kama maadui wa Urusi kwa kutamani wanajeshi wa Urusi kuuaana kwa maslahi yao, huku akiwashukuru maafisa wake wa usalama kwa kuhakikisha kuwa jaribio alillosema kujaribu kumwondoa uongozini linazimwa.

Wapiganaji wa Wagner wametakiwa kujiunga na jeshi la Urusi au wahamie nchini Belarus
Wapiganaji wa Wagner wametakiwa kujiunga na jeshi la Urusi au wahamie nchini Belarus REUTERS - STRINGER

Aidha, amewataka mamluki wa Wagner kuchagua kujiunga na jeshi la taifa, kwenda Belarus au kuamua kurejea nyumbani.

Kabla ya kusitisha jaribio la kutaka kuliondoa jeshi, kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin alitetea uamuzi wake akisema alitaka kuonesha mahaifu ya jeshi la Urusi, wala sio kumwondoa rais Putin madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.