Pata taarifa kuu

Putin: Uasi wa Wagner ni 'uhaini'

Nairobi – Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "uasi wa kutumia silaha" unaofanywa na  kikosi cha mamluki cha Wagner ni uhaini, na kwamba yeyote ambaye amechukua silaha dhidi ya jeshi la Urusi ataadhibiwa.

Rais wa Urusi Vladmir Putin anasema kitendo cha Wagner ni Uhaini
Rais wa Urusi Vladmir Putin anasema kitendo cha Wagner ni Uhaini via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa hotuba ya dharura iliyotangazwa kwenye televisheni, Putin alisema atafanya kila njia kuilinda Urusi, na kwamba "hatua madhubuti" itachukuliwa ili kuleta utulivu huko Rostov-on-Don, mji wa kusini ambapo mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin alisema kuwa vikosi vyake vimechukua udhibiti wa mitambo yote ya kijeshi.

Katika hotuba yake ya dharura, rais Putin amewataka wapiganaji wa Wagner kutomfuata mkuu wao
Katika hotuba yake ya dharura, rais Putin amewataka wapiganaji wa Wagner kutomfuata mkuu wao REUTERS - STRINGER

Mamlaka ya Moscow na maeneo jirani yanasema kuwa wametangaza hali ya hatari ya kukabiliana na ugaidi dhidi ya uasi wa kijeshi wa kiongozi wa mamluki wa Urusi Yevgeny Prigozhin.

"Ili kuzuia mashambulio ya kigaidi yanayowezekana katika jiji na mkoa wa Moscow, serikali imeanzisha oparesheni ya kukabiliana na ugaidi ," Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi ya Urusi ilisema.

Rais Putin ameahidi kupambana na Wagner
Rais Putin ameahidi kupambana na Wagner © REUTERS / STRINGER

Usalama umeimarishwa mjini Moscow. Eneo la Voronezh kusini magharibi mwa Urusi, ambalo linapakana na Ukraine, pia lilitangaza aina hii ya hali ya hatari.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema wapiganaji mamluki wa Kundi la Wagner "wamedanganywa na kuingizwa kwenye tukio la uhalifu" na mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin.

Katika taarifa iliyotumwa kupitia mtandao wa Telegram, wizara hiyo iliwataka wapiganaji wa Wagner kuwasiliana na wawakilishi wake na wale wa huduma za kutekeleza sheria, na kuahidi kuwahakikishia usalama wao.

Inadaiwa kuwa wapiganaji wa Wagner wamechukua baadhi ya maeneno ya Urusi yalioko karibu na Ukraine
Inadaiwa kuwa wapiganaji wa Wagner wamechukua baadhi ya maeneno ya Urusi yalioko karibu na Ukraine REUTERS - STRINGER

Kwa nini jeshi la mamluki la Wagner limeanzisha vita dhidi ya jeshi la Urusi

Mkuu wa kikosi cha mamluki cha Wagner cha Urusi Yevgeny Prigozhin alidai kuwa vikosi vyake vimeingia Urusi kuondoa uongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.

Idara za usalama za Urusi zilisema kuwa zilifungua uchunguzi wa jinai huko Prigozhin siku ya Ijumaa kwa kuanzisha kile wanachoelezea kama uasi.

Prigozhin kwa muda mrefu amekuwa akiwashutumu viongozi wakuu wa kijeshi wa Urusi kwa kushindwa katika vita vya Ukraine na anajulikana kwa uhasama wake wa muda mrefu na wizara ya ulinzi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.