Pata taarifa kuu

Ufaransa: Jengo moja laporomoka Paris, watu zaidi ya ishirini wajeruhiwa

Jengo lililokuwa likishika moto liliporomoka Jumatano Juni 21 katikati mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Polisi imesema mwanzoni mwa jioni watu wanne wako katika hali mbaya kabisa na wengine ishirini na watano wamelazwa hospitalini na wanaendelea vizuri. 

Moto mkubwa, ambao bado haujajulikana asili yake, ulizuka katika jengo moja katikati mwa jiji la Paris, ambalo sehemu moja ilidondoka mnamo Juni 21, 2023.
Moto mkubwa, ambao bado haujajulikana asili yake, ulizuka katika jengo moja katikati mwa jiji la Paris, ambalo sehemu moja ilidondoka mnamo Juni 21, 2023. AFP - ABDULMONAM EASSA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ofisi ya mashtaka, watu wawili wamekuwa wakitafutwa chini ya vifusi vya jengo hilo. Jumla ya maafisa 270 wa kikosi cha Zima moto wametumwa kwenye eneo la tukio pamoja na madaktari 9. Uchunguzi umefunguliwa kwa kuwajeruhi watu bila kukusudia, ofisi ya mashitaka imebaini.

"Ni ripoti ya muda", kwa sababu "bado kuna upekuzi chini ya vifusi" lakini moto "umedhibitiwa", ametangaza mkuu wa polisi, Laurent Nuñez, katika mkutano na waandishi wa habari karibu na eneo la tukio uliofanyika saa kui na mbili na nusu jioni. Maafisa 270 wa kikosi cha Zima moto wametumwa, ambao walikusanya mashine 70, "walizuia kuenea kwa moto huo kwa majengo mawili yaliyopakana ambayo yaliathiriwa sana na mlipuko" na watu "wamehamishwa", ameongeza. Kikosi cha Zima moto awali kiliripoti kuporomoka kwa majengo mawili. Lakini, kulingana na vyanzo vya polisi, ni jengo moja tu lililoporomoka.

Mwendesha mashtaka wa Paris, Laure Beccuau alieleza kuwa wachunguzi wawili kutoka mahakama wapo kwenye eneo la tukio. Uchunguzi wa majeraha bila kukusudia kwa kukiuka wajibu wa busara au usalama umefunguliwa, ofisi ya mashtaka imebainisha. "Milipuko ilisikika, bila kujuwa kwa wakati huu asili ya milipuko hiyo", ofisi ya mashitaka imeongeza.

Tukio hilo lilitokea kwenye mtaa wa Saint-Jacques, karibu na kanisa la Notre-Dame du Val-de-Grâce. 

Mkuu wa polisi wa Paris Laurent Nuñez alisema alikuwa "mwenye tahadhari sana" siku ya Jumatano kuhusu chanzo cha mlipuko huo.

Hii ni tathmini ya muda, kwa sababu bado kuna zoezi la kutafuta watu waliokwama  chini ya vifusi linalofanyika...

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.