Pata taarifa kuu

Ufaransa: Utaratibu wa haraka wa utambuzi wa majanga ya asili kuanzishwa na serikali

Siku ya Ijumaa, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.3 hadi 5.8 kulingana na Mtandao wa Kitaifa wa Ufuatiliaji wa Mitetemo (Renass) na Ofisi Kuu ya Seismolojia ya Ufaransa (BCSF) magharibi mwa Ufaransa.

"Kwa kuzingatia ukubwa wa tetemeko la ardhi lililopiga magharibi mwa Ufaransa, utaratibu wa kasi wa utambuzi wa majanga ya asili utaanzishwa ili kuzingatia uharibifu wa kimuundo ambao litasababisha", amesema waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa.
"Kwa kuzingatia ukubwa wa tetemeko la ardhi lililopiga magharibi mwa Ufaransa, utaratibu wa kasi wa utambuzi wa majanga ya asili utaanzishwa ili kuzingatia uharibifu wa kimuundo ambao litasababisha", amesema waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa. © Google Earth
Matangazo ya kibiashara

Baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea magharibi mwa Ufaransa Ijumaa jioni, serikali inachukua hatua za kwanza. Serikali itaanzisha utaratibu wa kasi wa kutambua majanga ya asili, ametangaza Waziri wa Mambo ya Ndani, Gérald Darmanin, kwenye Twitter, Jumamosi asubuhi.

"Kwa kuzingatia ukubwa wa tetemeko la ardhi lililopiga magharibi mwa Ufaransa, utaratibu wa kasi wa utambuzi wa majanga ya asili utaanzishwa ili kuzingatia uharibifu wa kimuundo ambao litasababisha", amesema waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, akiongeza "msaada wake kwa waathirika".

Tetemeko hilo kubwa lilitokea saa kumi na mbili na dakika 38 jioni katika mji wa Cram-Chaban (Charente-Maritime), karibu na Mauzé-sur-le-Mignon (Deux-Sèvres), katikati ya La Rochelle na Niort.

Kutoka Bordeaux hadi Rennes kupitia Limoges au La Rochelle, wakazi wengi walihisi dunia inatikisika na wito mwingi kwa maafisa idara ya Zima moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.