Pata taarifa kuu

Rafael Grossi, mkuu wa IAEA awasili katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhia nchini Ukraine

Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), amewasili katika kinu cha nyuklia cha Ukraine huko Zaporizhia, kinachokaliwa na vikosi vya Urusi. Rafael Grossi atatathmini hali baada ya uharibifu wa bwawa kwenye Mto Dnieper, ametangaza afisa wa Urusi leo Alhamisi, Juni 15.

Rafael Grossi katika eneo la nyuklia la Zaporizhia, Juni 15, 2023. Picha imepatikana kupitia AFP kutoka IAEA.
Rafael Grossi katika eneo la nyuklia la Zaporizhia, Juni 15, 2023. Picha imepatikana kupitia AFP kutoka IAEA. AFP - FREDRIK DAHL
Matangazo ya kibiashara

"Mkurugenzi Mkuu wa IAEA na timu yake wamewasili ZNPP", kifupi cha Kiingereza kinachotaja mtambo wa kuzalisha umeme wa Zaporizhia, Mikhail Ulyanov, mwakilishi wa kudumu wa Urusi kwa mashirika ya kimataifa huko Vienna, ameandika katika ukurasa wake wa Twitter. Rafael Grossi awali alipaswa kutembelea eneo hilo Jumatano ili kutathmini hatari zinazoweza kutokea kwa usalama kufuatia uharibifu wa bwawa la Kakhovka kwenye Mto Dnieper, ambalo maji yake hutumika kupoza vinu vyake sita ambavyo vimefungwa kwa sasa.

Ziara yaahirishwa

Lakini ziara hiyo ilikuwa imeahirishwa hadi Alhamisi, Juni 15 kwa sababu za kiusalama. "Haikuwa rahisi kuandaa ziara kama hiyo katika mazingira kama haya, lakini upande wa Urusi umefanya vyema," Bw Ulyanov amesema. Kinu cha nyuklia cha Zaporizhia, kikubwa zaidi barani Ulaya, kinakaliwa na jeshi la Urusi, ambalo linasimamia ziara ya Bwana Grossi.

'Nataka kufanya tathmini yangu mwenyewe'

Mkuu wa IAEA, ambaye tayari ametembelea mtambo huu mkubwa wa kuzalisha umeme mara kadhaa, atatambua hasa ikiwa umehatarishwa na uharibifu wa bwawa la Kakhovka. Kulingana na Bw. Grossi, hakuna "hatari ya haraka" kwa kituo hiki, lakini kiwango cha maji katika bonde la kupoeza kinamtia wasiwasi: "Kuna hatari kubwa kwa sababu kiwango cha maji yaliyo chini ni kidogo". "Nataka kufanya tathmini yangu mwenyewe," aliwaambia waandishi wa habari huko Kyiv siku ya Jumanne.

Kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhia kimekuwa kikilengwa mara kwa mara na milipuko ya mabomu, ambayo Moscow na Kyiv wanatuhumiana, na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wake.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.