Pata taarifa kuu

Belarus yaanza kupokea silaha za nyukilia za Urusi: Rais Alexander Lukashenko

NAIROBI – Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema nchi yake imeanza kupokea silaha za nyuklia za Urusi, ambazo anaeleza kuwa baadhi yake zina nguvu mara tatu zaidi ya mabomu ya atomiki ambayo yalitumika Hiroshima na Nagasaki mwaka 1945.

Rais wa Belarus  Alexander Lukashenko na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin © via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua ya kwanza ya Moscow kusafirisha silaha za nyuklia za masafa mafupi ambazo zinaweza kutumika kwenye uwanja wa vita - nje ya Urusi tangu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti.

Hatua hiyo inafuatiliwa kwa karibu na Marekani na washirika wake pamoja na China, ambayo imeonya mara kwa mara dhidi ya matumizi ya silaha za nyuklia katika vita vya Ukraine.

"Tuna makombora na mabomu ambayo tumepokea kutoka Urusi," Lukashenko alisema katika mahojiano na Rossiya-1, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na  serikali ya Urusi, ambayo yalichapishwa  kwenye mtandao wa Telegraph wa Shirika la Telegraph la Belarusi.

"Mabomu hayo yana nguvu mara tatu zaidi ya yale yaliyoangushwa Hiroshima na Nagasaki," alisema.

Haya yanajri wakati huu makombora ya Urusi yakiripotiwa kushambulia majengo ya kiraia katika bandari ya Odesa ya Bahari Nyeusi nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo, na kuua watu wasiopungua watatu na kujeruhi 13, jeshi la Ukraine limesema.

Urusi ilirusha makombora manne katika mji huo, kamandi ya kusini ya jeshi la Ukraine ilisema.

Aidha jeshi lilisema hapo awali kwamba makombora mawili yaliharibiwa kabla ya kutekeleza uharibifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.