Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron atoa wito wa kudhaminiwa usalama kwa Ukraine

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito siku ya Jumatano Mei 31 kwa ajili ya kutoa dhamana ya usalama "inayoonekana na ya kuaminika" kwa Ukraine, ikisubiri kujiunga na NATO, na kuomba ulinzi wenye nguvu zaidi wa Ulaya ndani ya Umoja huo, licha ya kujizuia kwa nchi nyingi za Ulaya ya Kati na Mashariki.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Bratislava, Mei 31, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Bratislava, Mei 31, 2023. © MICHAL CIZEK / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa tunataka [...] kuwa na uzito dhidi ya Urusi, ikiwa tunataka kuwa waaminifu kwa raia wa Ukraine, lazima tuipe Ukraine njia ya kuzuia uchokozi wowote mpya [wa Urusi] na kuzingatia usalama”, amesisitiza mkuu wa nchi wa Ufaransa Emmanuel Macron, wakati wa hotuba katika Mkutano wa 18 wa Usalama wa Kikanda wa Globsec huko Bratislava, ulioandaliwa na taasisi ya Think Tank ya jina moja. "Hii ndiyo sababu ninaunga mkono, na hili litakuwa mada ya majadiliano ya pamoja katika wiki zijazo, katika mkutano wa kilele wa Vilnius, wa kutoa dhamana inayoonekana na ya kuaminika ya usalama kwa Ukraine", amesema.

Mnamo Julai 11 na 12, Wakuu wa Nchi na Serikali wa NATO watathibitisha uungaji mkono wao wa kisiasa na kijeshi kwa Ukraine, ambayo imekumbwa kwa miezi kumi na tano na hujuma ya Urusi ambayo pia inatia wasiwasi nchi jirani zilizokuwa zamani sehemu za Umoja wa Kisoviet. Dhamana hizi zinaweza kutolewa na mataifa mbalimbali wanachama wa NATO, ikisubiriwa Ukraine kuingia katika Muungano huo, ambao utaendelea kuwa mbali sana maadamu iko vitani na Urusi. Wanaweza kupitia uwasilishaji wa silaha na teknolojia pamoja na mafunzo ya wanajeshi, hasa marubani wa ndee za kivita, uwezekano wa kuleta karibu na viwango vya NATO haraka iwezekanavyo.

"Lazima tujenge kitu kati ya usalama unaotolewa kwa Israeli [na Marekani] na uanachama kamili " katika NATO, amesisitiza Emmanuel Macron.

Upande wa mashariki, baadhi wanahofia kwamba ushirikiano usiotosha wa washirika wa Ukraine unaweza kusababisha kufungia mstari wa mbele wa sasa na kuunganisha mafanikio ya eneo la Urusi bila kuleta amani. "Mgogoro uliozuiwa unaweza kuwezesha Urusi tu kujiandaa kwa uchokozi mwingine," asema Slawomir Debski, mkurugenzi wa Taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Poland (PISM).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.