Pata taarifa kuu

Tutatumia nguvu kubwa kuwakabili wavamizi kutoka nje : Urusi

NAIROBI – Urusi imeonya kuwa itatumia nguvu kubwa kuwakabili wavamizi kutoka nje iwapo wataingia tena kwenye ardhi yake, onyo linalokuja baada ya kutumia ndege zake za kivita kushambulia kundi lilolikuwa limejihali katika jimbo la Belgorod.

Vladimir Putin, Rais wa Ukraine Tarehe 23 Mei 2023.
Vladimir Putin, Rais wa Ukraine Tarehe 23 Mei 2023. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limetolewa na waziri wa ulinzi Sergei Shoigu wakati wa mazungumzo na wakuu wa jeshi na kudai kuwa makabiliano dhidi ya kundi hilo la kigeni aliloliita magaidi kutoka Ukraine, yalisababisha vifo vya watu 70.

Mbali na mauaji hayo, Urusi inadai kuwa ilifanikiwa kuharibu magari ya kijeshi ya kundi hilo, ambalo hata hivyo Ukraine imekanusha kuhusika.

Urusi pia inadai kuwa watu waliovamia ardhi yake, walitumia magari ya kivuta kutoka nchi za Magharibi hasa Marekani, lakini shutuma hizo zimekanuswa vikali huku wachambuzi wa mzozo huu wakisema huenda Moscow imeigiza tukio hilo.

Katika hatua nyingine, akizunguimzia kuhusu mapigano yanayoendelea nchini Ukraine, Shoigu amesema Uurusi iliwalipa fidia ya hadi Dola Elfu 62 kwa  família za wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa katika vita hivyo.

Wakati hayo yakijiri, uongozi wa kundi la Wagner linaloisaidia Urusi katika mapigano nchini Ukraine umesema, wafungwa karibu Elfu 10 waliotumwa katika uwanja wa vita wameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.