Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ujerumani na Uturuki zaingia katika mzozo wa kidiplomasia

Kampeni za uchaguzi nchini Uturuki, kabla ya duru ya pili Jumapili Mei 28, zinazusha mvutano wa kidiplomasia kati ya Ujerumani na Uturuki. 

Bendera za Ujerumani na Uturuki zinapepea katika uwanja wa ndege wa Tegel mjini Berlin Septemba 27, 2018, kabla ya ziara ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Bendera za Ujerumani na Uturuki zinapepea katika uwanja wa ndege wa Tegel mjini Berlin Septemba 27, 2018, kabla ya ziara ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Berlin, Pascal Thibaut

Ankara ilishutumu misako iliyofanywa katika nyumba za waandishi wa habari wa Uturuki nchini Ujerumani na kumwitisha balozi wa Ujerumani. Jumatatu, Mei 21, balozi wa Uturuki mjini Berlin ambaye pia aliitishwa na mamlaka ya Ujerumani ambayo haikufurahishwa na ukosoaji mkubwa wa Ankara iliyobaini kwamba uhuru wa vyombo vya habari ulihatarishwa.

"Uvamizi wa polisi uliondaliwa na Ujerumani ambayo inalinda magaidi": Gazeti la kila siku la Uturuki la Sabah, linalomilikiwa na mshirika wa karibu wa Rais Recep Tayyip Erdogan, liliripoti siku chache zilizopita, baada ya upekuzi kwenye nyumba za wafanyakazi wawili wa magazeti karibu na Frankfurt. Mahakama moja ya Ujerumani iliwashutumu kwa kuchapisha katika ukurasa wa mbele, mwaka jana, anwani ya mpinzani wa Uturuki anayeishi Ujerumani na ambaye chaneli yake ya YouTube ni maarufu sana.

Ankara inamtuhumu mpinzani na mkosoaji huyo wa Rais Erdogan chini ya ulinzi wa mahakama kwa kumuunga mkono mhubiri Fethullah Gülen, anayeshutumiwa na Uturuki kwa kuchochea jaribio la mapinduzi lililoshindwa katika majira ya joto ya mwaka 2016.

Wasiwasi unaohusishwa na kampeni ya uchaguzi na uwepo wa wapiga kura milioni 1.5 wa Uturuki nchini Ujerumani unaeleza kwa nini misako hiyo ilisababisha athari ya kidiplomasia. Ankara ilimwitisha balozi wa Ujerumani wiki iliyopita kushutumu "vitisho vya vyombo vya habari vya Uturuki". Jumatatu, Mei 21, balozi wa Uturuki nchini Ujerumani ambaye aliitishwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Berlin, na kufutilia mbali shutuma za Ankara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.