Pata taarifa kuu

Urusi inasema imefanikiwa kuwaondoa watu waliokuwa wamevamia ardhi yake

NAIROBI – Urusi inasema wanajeshi wake, wamewashinda na kuwaondoa kundi la watu lenye silaha inalosema lilikuwa na mchanganyiko wa jeshi la Ukraine, lilivuka mpaka na kuingia katika jimbo lake la Belgorod Kusini mwa nchi yake. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin © via REUTERS / SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi nchini Urusi inaishtumu Ukaine kwa kupanga mashambulio katika ardhi yake, na hivyo ililazimika kutumia ndege na magari ya kivita kuwasambaratisha. 

Hata hivyo, Ukraine imeendelea kukanusha madai hayo ya Urusi na badala yake kudai kuwa kundi hili limepangwa na Urusi yenyewe. 

Aidha, Jeshi la Urusi linadai kuwa limewauwa wapiganaji zaidia ya 70 kutoka Ukraine walioshambulia ardhi yake kwa magari ya kijeshi. Moscow imeelezea kitendo hicho kama cha kigaidi. 

Katika hatua nyingine, rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametembelea wanajeshi wa nchi yake katika mstari wa mbele wa mapambano katika jimbo la Donetsk, baada ya ziara yake nchini Japan na Saudi Arabia. 

Umoja wa Ulaya, nao umeanza kutoa mafunzo maalum kwa marubani wa kijeshi wa Ukraine namna ya kupambana kwa kutumia ndege aina ya F 16, mazoezi ambayo yanaendelea nchini Poland, kwa mujibu wa Josep Borrell, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.