Pata taarifa kuu

Urusi imetoa hati ya kukamatwa mwendesha mashtaka wa ICC karim Khan

Moscow imetoa hati ya kukamatwa kwa mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ambaye mwezi Machi alitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, vyombo vya habari vya Urusi viliripoti Ijumaa.

Karim Khan, mwendesha mashtaka wa ICC anatakiwa na Urusi
Karim Khan, mwendesha mashtaka wa ICC anatakiwa na Urusi © AP/Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Karim Khan, mwendesha mashtaka katika mahakama ya uhalifu wa kivita yenye makao yake makuu The Hague, aliongezwa kwenye orodha ya watu wanaotakiwa na wizara ya mambo ya ndani, ya Urusi.

Shirika la habari la Urusi la TASS liliripoti Ijumaa, likinukuu hifadhidata ya wizara hiyo.

Picha ya mwendesha mashtaka wa ICC, ambaye ni raia wa Uingereza, iliaanza  kuonekana kwenye hifadhidata ya wizara ya mambo ya ndani ya Urusi siku ya Ijumaa, kulingana na ripoti za habari.

Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, ambayo inashughulikia uhalifu mkubwa, ilisema mwezi Machi kwamba Khan alikuwa anachunguzwa kwa kuaagiza mashtaka ya jinai kwa mtu ambaye kuwa hana hatia" - akimaanisha mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Putin.

Mwendesha mashtaka wa ICC pia alikuwa anachunguzwa kwa madai ya kuandaa "shambulio dhidi ya mwakilishi wa taifa la kigeni ambalo lipo chini ya ulinzi wa kimataifa", wachunguzi wa Urusi walisema wakati huo.

Mnamo Machi 13, 2022, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Karim Khan (katikati, akizungumza na mwendesha mashtaka mkuu wa wakati huo wa Ukraine Iryna Venediktova) huko Bucha, ambako wanajeshi wa Urusi wanashukiwa kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Mnamo Machi 13, 2022, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu Karim Khan (katikati, akizungumza na mwendesha mashtaka mkuu wa wakati huo wa Ukraine Iryna Venediktova) huko Bucha, ambako wanajeshi wa Urusi wanashukiwa kufanya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. © Fadel Senna/AFP

Notisi iliyotafutwa ilimtaja Khan kuwa ni mtu aliyezaliwa Machi 30, 1970 huko Edinburgh, Scotland lakini hakutaja kosa lake.

Urusi ilimfungulia Khan kesi ya jinai baada ya mahakama ya ICC kutangaza hati ya kukamatwa kwa Putin kwa tuhuma za kutenda uhalifu wa kivita kwa kuwasafirisha kinyume cha sheria maelfu ya watoto wa Ukraine na kuwapeleka Urusi.

ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladmir Putin
ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladmir Putin AP - Gavriil Grigorov

Mahakama ya kimataifa pia ilitoa hati ya kukamatwa kwa Maria Lvova-Belova, kamishna wa rais wa Urusi anayeshughulikia haki za watoto.

Kyiv anasema zaidi ya watoto 19,000 wa Ukraine wamefukuzwa nchini Urusi tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Moscow mnamo Februari 2022, na zaidi ya 4,000 wanaaminika kuwa yatima. Wengi wanadaiwa kuwekwa katika taasisi na nyumba za watoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.